Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikiongoza kikao cha
pamoja kati ya Uongozi wa Shirika la Microsoft na Watendaji wa
Mawasiliano, Sayansi na Elimu ya Juu wa SMT Na SMZ kilichofanyika
katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo ndani ya jengo la Bunge
Mjini Dodoma.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ
***************************************
Shirika
la Kimataifa la Mitandao ya Mawasiliano la Microsoft linakusudia
kuendesha mradi maalum na Tanzania wa kuwasaidia wanafunzi wa Vyuo
Vikuu Nchini Tanzania { Broard Band } katika masomo yao kupitia mfumo
wa kisasa wa mtandao wa Internet.
Mfumo
huo mpya utamuwezesha kila mwanafunzi wa chuo Kikuu kufikia hatua ya
kuwa na Laptop yake itakayoambatana na vifaa vyake vikijumuisha pia
huduma za mtandao wa Internet ili kumrahisishia masomo yake.
Makamu
wa Rais wa Shirika la Microsoft lenye Makao Makuu yake Mjini Seattle
Nchini Marekani Bw. David Tennenhouse alieleza hayo katika kikao cha
pamoja kati ya Uongozi wa Shirika lake na Watendaji wa Taasisi za
Sayansi, Mawasiliano ya Elimu ya juu Bara na Zanzibar kilichofanyika
kwenye ukumbi wa Ofisi ya waziri Mkuu iliyopo ndani ya Jengo la Bunge
Mjini Dodoma.
Kikao
hicho kilichokuwa chini ya mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kimekuja kufuatia ziara yake aliyoifanya
katika Mji wa Seattle Nchini Marekani wiki chache iliyopita ambapo
Uongozi wa Microsoft uliahidi kufika Tanzania kwa mazungumzo zaidi ya
ushirikiano kati ya pande hizo mbili.
Bwana
David Tennenhouse aliwaeleza wajumbe wa kikao hicho kwamba Microsoft
tayari imeshatiliana saini Mkataba na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania {
Costec } kwa ajili ya kuendesha mradi huo wa Braord Band.
Alifahamisha
kwamba awamu ya kwanza ya mpango huo maalum inaanzia kwa wanafunzi wa
chuo kikuu cha Dar es salaam na baadaye kuendelea na vyuo vyengine vikuu
vya Tanzania.
Kwa
Zanzibar mpango huo utajumuisha vyuo vikuu vya SUZA, Tunguu, Chukwani
vikiwemo pia chuo cha Ufunsi Mbweni, Chuo cha Elimu ya Afya Mbweni, Chuo
cha Uongozi wa Fedha Chwaka pamoja na Chuo cha Kiislamu Mazizini.
Makamu
wa Rais wa Shirika hilo la Microsoft alieleza kwamba makubaliano yao
mengine ya msingi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania { Costec }
yanahusisha pia mradi wa kusaidia walimu kufundisha mitaala ya Kompyuta {
T 21 }.
Akitoa
shukrani zake kwa Shirika hilo la Microsoft Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameupongeza uongozi wa Taasisi hiyo kwa
hatua iliyochukuwa katika kipindi kifupi mara tu baada ya ziara yake ya
hivi karibuni Nchini Marekani ambapo pia alipata nafasi ya kutembelea
Ofisi za Shirika hilo Mjini Seattle.
Balozi
Seif alisema Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania
na ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia washirika wa maendeleo zimekuwa
zikifanya jitihada za kuwajengea mazingira bora ya kitaaluma wanafunzi
wake kupitia mfumo mpya wa mawasliano ili wawe na uwezo kamili wa
kuhimili mabadiliko ya teknolojia yaliyopo hivi sasa Duniani.
Katika
Kikao hicho watendaji wa Taasisi za Mawasiliano, sayansi na Elimu ya
Juu ya SMT na SMZ wameuomba uongozi wa shirika hilo la Microsoft
kusaidia uanzishwaji wa kituo cha utengenezaji wa mawasiliano { IT Park
} pamoja na ulinzi kwenye mitandao kwa ajili ya kuwaepusha watoto na
wanafunzi kuingia katika mmong’onyoko wa maadili.
Katika
Kikao hichowatendaji wa Taasisi za Mawasilino, Sayansi na Elimu ya juu
Tanzania Barana na Zanzibar wameuomba Uongozi wa shirika hilo la
Microsoft kusaidia uanzishwaji wa kituo cha utengenezaji wa mawasiliano{
IT Park } pamoja na ulinzi kwenye mitandao kwa ajili ya kuwaepusha
watoto na wanafunzi kuingia katika mmong’onyoko wa maadili.
Pia
waliomba huduma za misaada na taaluma kwenye E Government, mpango
maalum wa ulinzi wa Mkongo wa Taifa pamoja na mradi wa kukusanya vijana
kuwashajiisha ili waweze kujiendeleza zaidi kimaisha.
Wakati
huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alikutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Kazi Ulimwenguni { ILO } Bwana Guy Ryder hapo Ofisini kwake Mtaa wa Vuga
Mjini Zanzibar.
Katika
mazungumao yao Balozi Seif aliushauri Uongozi wa Shirika hilo
kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika harakati
zake za kujikwamua katika vikwazo vya kiuchumi likiwemo tatizo la
ajira kwa watoto.
Alisema
kazi kubwa iliyopo hivi sasa ni kuwajengea mazingira bora ya kitaaluma
watoto pamoja na kundi la Vijana kwa lengo la kukabiliana vyema na
fursa za ajira ambazo nyingi zinazohitaji kiwango kikubwa cha elimu
hupatikana katika Taasisi, Jumuiya na Mashirika Binafsi.
“
Zipo fursa nyingi za ajira hasa katika taasisi, jumuiya na mashirika
binafsi lakini mara nyingi kinachojitokeza kwa vijana walio wengi hapa
nchini ni kuwa na ufinyu wa taalamu “ Alisisitiza Balozi Seif.
Mapema
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi la Kimataifa { ILO } Bwana Guy
Ryder alisema mataifa mengi duniani yakiwemo pia yale yaliyoendelea
bado yanakabiliwa na changa moto kubwa za ajira hasa kwa Vijana.
Bwana
Ryder alisema changamoto hiyo inasababishwa na ukosefu wa taaluma kwa
Vijana hao jambo ambalo shirika lake litajitahidi kuona taaluma hiyo
inawafikia wahusika hao ili wawe za uwezo wa kujiajiri wenyewe badala ya
kutegemea ajira za Serikali.
Mkurugenzi
huyo wa Shirika la Kimataifa la Kazi ulimwenguni { ILO } aliipongeza
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa ushirikiano mzuri inayotoa kwa shirika hilo hasa katika
kukabiliana na ajira za watoto.
Bwana
Guy Ryder alimuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Shirika
hilo litaendelea kusaidia Serikali hizo katika kuona watoto
wanaotumikishwa katika kazi mbali mbali wanaachana nazo ili baadaye
warejee maskulini.
Mkurugenzi
Mkuu huyo wa Shirika la Kimataifa la Kazi Ulimwneguni { ILO } alikuwepo
Nchini Tanzzania kwa ziara ya siku Nne kutembelea na kuona Programu na
miradi inayosimamiwa pamoja na kufadhiliwa na shirika hilo.
Post a Comment