SULEIMAN RAJABU.
******
Na Imelda Mtema
MASKINI! Yule mtoto Suleiman Rajab aliyeteseka muda mrefu akisumbuliwa na uvimbe mkubwa mguuni huku mamia ya Watanzania wakijitolea kuchanga fedha kwa ajili ya matibabu nchini India amefariki dunia ghafla nyumbani kwao Ukonga-Kivule, Dar.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa baada ya kifo hicho, baba mzazi wa marehemu, Rajab Upinde alisema kwamba mtoto wake huyo hakuwa anasumbuliwa na kitu chochote zaidi ya uvimbe uliokuwa mguuni lakini alishikwa na ugonjwa wa ghafla na kufariki dunia.

Baba huyo alisema kwamba Kampuni ya Global Publishers kwa kushirikiana na Hoyce Temu kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania kwenye Runinga ya Chanel Ten walifanya jitihada kubwa za kukusanya michango ambayo ilifanikisha maandalizi ya safari ya matibabu India.
“Naumia sana kwa vile kila kitu kilikuwa tayari. Tulikuwa tunasubiri siku ya kuondoka tu. Global Publishers na Hoyce wamefanya kazi kubwa kukamilisha safari ya India lakini ndiyo hivyo Mungu kampenda zaidi kiumbe wake,” alisema baba huyo kwa uchungu.
Akizungumzia kifo cha mtoto wake, baba huyo alisema kuwa siku ya tukio Sele aliamka akilalamika kichwa kinamuuma ambapo walimpa dawa za kutuliza maumivu.
Alisema aliporejea kutoka kazini mkewe alimwambia kuwa Sele alikuwa akilalama kuwa miguu inawaka moto ambapo alimfuata mwanaye chumbani ambaye aliomba aitiwe shehe.Shehe alipofika alimuombea na baada ya muda aliwaita wadogo zake na kuwaambia yeye anakufa kwani anajisikia vibaya mno.
Baba huyo aliendelea kusema kuwa akiwa amekaa nje alisikia mwanaye mwingine akimuita aingie ndani kwani hali ya Sele ilikuwa imebadilika na alipoingia alimkuta mwili wote umelegea ambapo aliita majirani ili wamsaidie, walipoingia ndani walimkuta ameshafariki dunia.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
“ Ki ukweli sikuweza kuamini macho yangu kama mwanangu ndio ameniaga kwani nilikuwa na ndoto nyingi za kumuona akipona tena na kuwa mzima kama walivyo watoto wengine” alisema baba huyo.
Kampuni ya Global Publishers kwa kushirikiana na kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa kupitia Televisheni ya Channel Ten na mwanadada Hoyce Temu, na kwa watanzania wote walio nje ya nchi kwa kujitahidi kutoa michango yao Mungu awabariki sana.
VIA GPL
Post a Comment