Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HII HAPA LIST KAMILI YA MARAIS WATAKAOHUDHURIA MAZISHI YA MANDELA

MARAIS  91 akiwemo Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa viongozi  wengine kutoka pembe zote ulimwenguni wanaotarajiwa kuhudhuria ibada ya  wafu ya aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Jumanne mjini  Johannesburg.

Huo unatarajiwa kuwa mkusanyiko mkubwa zaidi kuwahi  kushuhudiwa katika karne hii, ambapo marais wanne wa Amerika  watahudhuria. Itakuwa pia mara ya kwanza kwa  marais wanne wa Amerika  katika kipindi cha miaka 15 kuhudhuria hafla ya aina hiyo kwa pamoja.
  
Rais  Kenyatta aliondoka Kenya mwendo wa saa kumi na mbili jioni Jumatatu  kuelekea Afrika Kusini. Kwa mujibu wa Chumba cha Habari cha Rais (PSCU),  Rais Kenyatta aliyeandamana na mkewe Margaret aliagwa uwanja wa ndege  na Naibu Rais William Ruto.
   


    Mandela  ameombolezwa ulimwenguni kote katika makanisa, misikiti na masinagogi na  kupelekea maombolezo yake kuwa ya kipekee kuwahi kuunganisha makabila  na dini zote ulimwenguni.
   
Maombolezo yake  yanaweza kulinganishwa na ya aliyekuwa Rais wa Amerika J F Kennedy,  aliyeuawa mnamo 1963, na yale ya Binti Mfalme Diana aliyefariki kwenye  ajali ya barabarani mnamo Agosti 31, 1997. Mengine ni ya Papa John Paul  wa Pili aliyefariki mnamo 2004 na kuombolezwa ulimwenguni kote.
   
    Mazishi  ya Mandela yatahudhuriwa na Rais Barack Obama na mkewe Michelle,  waliokuwa marais George Bush, Bill Clinton na Jimmy Carter. Rais Obama,  mkewe Michelle na aliyekuwa Rais George Bush na mkewe Laura waliondoka  Jumanne Amerika kuelekea Afrika Kusini.
   
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki-Moon pia atahudhuria.
   
Waziri  Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu hatahudhuria mazishi ya Hayati  Nelson Mandela kwa sababu ni ghali mno kusafiri hadi nchini Afrika  Kusini, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari.
   
    Awali,  Bw Netanyahu alikuwa amefahamisha serikali ya Afrika Kusini kuwa  angehudhuria mazishi hayo lakini akafutilia mbali safari hiyo katika  dakika ya mwisho.
   
    Kulingana na redio ya  taifa la Israeli, waziri  huyo itatumia kiasi cha 7.0 milioni shekels  ambazo ni sawa na Sh170 milioni kusafiri nchini Afrika Kusini pamoja na  walinzi  wake:  “Uamuzi huo umeafikiwa kutokana na gharama kubwa ya  usafiri kwani safari hiyo ilipangwa katika kipindi cha muda mfupi,”  ikasema radio ya taifa, Haaretz.
   
    Kiongozi  huyo wa Israeli amekuwa akishutumia na raia wa nchi hiyo kuwa amekuwa  akitumia zaidi ya dola $1 milioni kuendesha shughuli za kasri zake  tatu. Vyombo vya habari vilidokeza kuwa kiongozi huyo hutumia fedha za  walipa ushuru dola $23,000 kulipia maji  ya kujaza mabwawa ya maji.
   
    Zaidi  ya viongozi 70 kutoka kote duniani tayari wamethibitisha kuwa  watasafiri kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mazishi ya hayati  Nelson  Mandela.
   
    Kwa upande wake, mbali na kuwa  shujaa ulimwenguni, Mandela pia anaashiria mwanzo mpya Afrika kwa kuleta  pamoja kwa mara ya kwanza kongamano kubwa la viongozi ulimwenguni kando  na Umoja wa Mataifa au Umoja wa Afrika.
   
Maishani  mwake hadi kufariki kwake, Mandela ameweza kuendeleza ulimwengu. Maisha  yake, kuanzia kufungwa kwake gerezani, kuchukua hatamu ya urais,  kustaafu, hadi kufariki kwake, kumefanyika wakati ambapo kuna maendeleo  makubwa ya kiteknolojia.
   
Mbali na  televisheni na redio, magazeti na mitandao ya kijamii imeeneza habari  kumhusu kwa kiwango kikubwa. Teknolojia imewezesha ulimwengu kuweza  kuomboleza kwa pamoja, huku kila mmoja akiweza kuamua kuhusu watu  wanaostahili kuombolezwa kwa taadhima kuu.
   
    Hadhi  kubwa inayoonekana katika maombolezo ya Mandela, ikiwemo idadi kubwa ya  viongozi wa kitaifa wanaotarajiwa kuhudhuria, huenda isifikiwe na  viongozi wengine katika karne hii.
   
    Mandela,  ambaye amecha watoto sita, wajukuu 17 na vitukuu 14, atazikwa nyumbani  kwao Qunu, Cape Mashariki, Jumapili, Desemba 15. --- SwahiliHub.com

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top