Watu 250 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Tawi la Kigunga B, Kilakala wilayani Temeke jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi kadi kwa
wanachama wapya, Katibu wa Vijana wa CCM, wilayani Temeke Onesha Haruna
amesema viongozi wa chama hicho wana jukumu kubwa la kuhakikisha idadi
ya wanachama inaongezeka kila kukicha.
Hili litafanikiwa ikiwa kila mmoja wao atatekeleza
ilani ya chama chao kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na kufanya
uhamasishaji kwa watu mbalimbali.
“Ilani ya CCM haina mapungufu hata chembe. Ikiwa
itafuatwa na kutekelezwa kila kilichoandikwa ndani yake, ni wazi kuwa
chama chetu kitakuwa chama cha mfano na chenye kuongoza kwa idadi ya
wanachama kuliko hata ilivyo sasa” alisema.
Licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo za
ndani kama vile kuwepo kwa makundi ndani ya chama, bado kimeonyesha
kuimarika zaidi kutokana na kuwa na viongozi wenye moyo madhubuti wa
kukiongoza.
Katika hotuba yake, Haruna alitoa wito kwa
wenyeviti wa vijana katika matawi ya wilaya hiyo kuhamasisha makundi ya
vijana kujiunga na CCM.
“Vijana ni taifa la leo, hivyo kuwa na ushiriki
mkubwa ndani ya chama, kuwezesha kupatikana kwa maendeleo kwani siku
zote chama ni watu,” alisema Haruna.
MWANANCHI
MWANANCHI
Post a Comment