Mwenyekiti wa kamati hiyo, Rajab Mohammed Mbarouk (pichani), alisema katika kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli zingine za kawaida za halmashauri, imebainika kwamba upo mtindo wa Serikali kutuma katika halmashauri kiasi kikubwa cha fedha kuliko kiasi kilichoidhinishwa na Bunge.
“Aidha fedha zinazopelekwa katika halmashauri si halali kwani hazijaidhinishwa na Bunge lako Tukufu ambalo hupitisha mafungu ya serikali,” alisema.
Pia alisema lipo tatizo lingine la kuzipelekea halmashauri kiasi kidogo cha fedha ikilinganishwa na kiasi halisi kilichoombwa ama kuidhinishwa.
Alisema madhara yake ni kwamba miradi husika hutekelezwa nusu nusu, chini ya viwango na nje na ratiba za uekelezaji wa miradi husika.
Taarifa ya kamati hiyo imelalamikia kitendo cha watumishi wanaotuhumiwa kufanya ubadhirifu katika halmashauri moja kisha kuhamishwa haraka vituo vingine na baadhi yao Tamisemi kuthubutu kuwapandisha vyeo. Masasi,” alisema.
Alisema kamati imekuwa Tamisemi imekuwa ikitumia mtindo huu wa kuwalinda watumishi mafisadi ndani ya halmashauri na kuifanya kamati iamini kuwa Tamisemi ni sehemu ya ufisadi huu na kwa makusudi mazima imekuwa ikieneza saratani hiyo kwenye halmashauri nyingi iwezekanavyo.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment