KATIBU Mkuu mpya wa TFF, Selestine
Mwesigwa ameingia ofisini na mkakati ambao hakuna tajiri yeyote wa Simba
wala Yanga atataka kuusikia. (HM)
*******
Kama mkakati huo utafanya kazi hakuna
fedha zozote za mashabiki au wanachama matajiri zitatumika kufanya
vurugu za usajili, jambo ambalo huenda likashitua wengi.
Yanga na Simba zimekuwa zikifanyiana
vurugu kwa kupokonyana wachezaji wakati wa usajili huku wanachama
matajiri ambao wengine si viongozi wakitaka kutunishiana ubabe na
kuonyeshana nani mwenye fungu.
Lakini Mwesigwa ameingia TFF na mfumo
ambao utazizuia klabu kutumia fedha yoyote ambayo haitokani na soka kama
zilivyozowea kufanya Simba na Yanga ambazo hazina vyanzo maalum vya
mapato.
Kwa mujibu wa Mwesigwa klabu zote za
Ligi Kuu Bara zitatakiwa kujihadhari na matumizi ya fedha ambazo
hazitokani na soka katika matumizi yake mbalimbali
ikiwemo usajili.
ikiwemo usajili.
Mwesigwa aliliambia Mwanaspoti kwamba,
moja ya mambo ambayo atayasimamia ni utekelezaji wa azimio la Bagamoyo
ambalo lilielekeza mambo kadhaa ya kufuatwa ili kuendeleza soka nchini
miongoni mwa mambo hayo ni klabu kuwa na watumishi wenye sifa, viwanja
vya mazoezi na uwazi katika taarifa za mapato na matumizi.
Katika mapato na matumizi ndipo
inapoingia hoja ya kuwepo kwa matumizi ya haki ya fedha za soka yaani
'Football Financial Fairplay', mfumo ambao unasimamiwa na Shirikisho la
Soka Ulaya (Uefa).
"Football Financial Fairplay ndiyo
itakayoongoza klabu kutumia fedha zinazotokana na soka tu na si
vinginevyo, unajua hapa ndipo mambo yanapoharibika kwani unaweza kuona
klabu moja inaidhamini klabu nyingine na kupunguza ushindani katika
ligi," alisema Mwesigwa ambaye ni mtaalam wa uongozi wa biashara.
Mwesigwa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa
Yanga, alisema hata kama klabu zinasaidiwa na watu wenye fedha misaada
hiyo inatakiwa kuwepo katika mikataba maalum na si mtu au kundi la watu
binafsi kuingiza fedha kienyeji kwenye timu.
Klabu za Simba na Yanga mara nyingi
zimekuwa zikifanya usajili wa wachezaji wake kwa kutumia mamilioni ya
fedha ambazo hutoka kwa wapenzi na wanachama wake.
"Unajua hata Uefa baada ya kuona
baadhi ya timu zinakuwa juu na nyingine zinaelekea kufa wakaanzisha hii
'Football Financial Fairplay' ili kuzipa nguvu na klabu nyingine, hivyo
na mimi nitaisimamia ili kuona tunapiga hatua katika soka," alisema
Mwesigwa mwenye umri wa miaka 43.
Hiyo inamaanisha kwamba kama klabu
itataka kusajili itapaswa kutumia fedha zake yenyewe au ambazo
zimetokana na udhamini ambao upo kwenye makubaliano maalum na si
mwanachama au shabiki kutoa fungu ghafla. Chanzo: mwanaspoti
Post a Comment