Wananchi wa Zanzibar wametakiwa kuelewa hali ya amani iliopo hivi sasa katika visiwa hii imetokana na mchango mkubwa wa viongozi wawili ambao ni wazalendo wa nchi hii akiwa ni Raisi mstaafu Mh,Amani karume pamoja na Maalim Seif.
Shauri hilko limetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya maridhiano Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo ambae pia aliwahi kuwa mwanasheria katika zama za mwanzo za utawala wa Mzee Karume katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Wananchi CUF uliofanyika Jimbo la Chaani hapo jana.
Mzee Moyo alisema Wazanzibar wanaposimama kudai urai wao pamoja na mambo mbali mbali ambayo yanaweza kuwaletea maendeleo ya hali ya juu katika nchi yao kuwa sio kosa kwani hapo awali Zanzibar iliweza kujiendesha wenyewe bila ya kuwepo kwa muungano.
Alisema kupitia mchakato wa katiba mpya ambayo wananchi wa Zanzibar wamedai mambo kadhaa yasiwe ya Muungano ambayo yatawawezesha Wazanzibar wenyewe kuwa huru kufanya wanachokitaka kwa maslahi ya Taifa lao,kufanya hivo sio kosa isipokuwa ni uhuru wa kila mwananchi kuamua anachokitaka kwa nchi yake.
Alieleza kazi kubwa ya kamati ya maridhiano Zanzibar ni kuhakikisha kuwa inaondosha chuki,ubaguzi na kila aina ya mfarakono. Ndani ya visiwa hivi ambapo kwa makusudi wamekuwa wakitokea baadhi ya watu kupandikiza chuki kwa wazanzibar.
‘’Tutahakikisha kuwa kila mzanzibar anaelewa lengo letu kwa nchi hii’’ alisema Mzee Moyo.
1 comments:
Rais Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa Mhe James Mbatia
ReplyPost a Comment