Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na tukio la ujambazi mkoani Singida.
Na Nathaniel Limu, Singida
MFANYAKAZI
wa Hoteli ya kitalii ya Lake Hill Singida Motel iliyopo mjini hapa
pamoja na walinzi watatu wa kampuni ya ulinzi ya binafsi wanashikiliwa
na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kuvamia hotel ya Lake Hill Singida
Motel na kisha kupora wapangaji wawili mali mbali mbali pamoja na fedha
taslimu.
Mfanyakazi
wa Lake hill hotel anayeshikiliwa ni Alistided Salvatory (24) na
wengine ambao ni walinzi wa kampuni binafsi ya Mass Security, ni Jumwa
Mwangwi (35), Zakaria Pstory (23) na Donald Samsoni (19).
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio
hilo la uporaji limetokea Desemba tisa mwaka hu saa 9:30 usiku huko
hotel ya Lake Hill Singida motel.
Alitaja
wapangaji walioporwa mali zao kuwa ni Alex Fabian (59) mkazi wa Mbweni
na raia wa Pakistani Rohan Yakubu (44) ambao inaelekea walikuwa
wamelengwa.
“Vitu
vilivyoporwa ni simu tatu za mkononi zenye thamani ya shilingi
1,020,000= saa mbili za mkononi moja yenye thamani ya dola 500 za
marekani, (nyingine thamani bado haijajulikana).Pia wamepora fedha
taslimu 800,000/= na dola za kimarekani 500”,alisema.
Akifafanua
juu ya uporaji huo, Kamwela amesema siku ya tukio watu wanaosadikiwa
kuwa ni majambazi ambao idadi yao bado haijajulikana wakiwa na bunduki
walivamia hoteli hiyo na kisha kufanya uporaji.
Amesema
watu hao walipofika katika hotel hiyo walifyetua risasi hewani kwa
lengo la kuwatisha wapangaji na walinzi waliokuwa kwenye hoteli hiyo. “Walifanikiwa
kuwafunga kamba ya katani walinzi wote watatu na hatimaye kuingia
katika vyumba viwili na kufanya unyang’anyi huo”,alifafanua zaidi.
Post a Comment