Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

VIOJA VILIVYOJITOKEZA MPAKA SASA MSIBA WA MANDELA

 

mkalimaniMKALIMANI aliyekuwa akitafsiri lugha kwa alama wakati wa shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mpigania uhuru na haki za watu weusi wa nchi hiyo, Nelson Mandela, amegunduliwa kuwa alikuwa feki.
Hayo yalibainishwa na mkurugenzi wa taifa wa shirikisho la watu wenye ulemavu wa kusikia wa nchini humo, Bruno Druchen, alipokuwa akizungumza na wanahabari na kuwaambia kuwa alimgundua kutokana na namna alivyokuwa akiizungusha mikono yake kama mtu asiyejua lolote.
Druchen alisema, “Nilimuona akizungusha mikono yake, lakini haikuwa ikimaanisha lolote kwa watu wenye ulemavu.”

Druchen alisema kuwa mkalimani huyo alikuwa amesimama karibu na Rais Barack Obama huku akitoa tafsiri ambazo kimsingi hazikuwa na maana ile iliyokuwa ikimaanishwa.
Naye mke wa Druchen ambaye ni mbunge wa Afrika Kusini kwa upande wa watu wenye ulemavu, Wilma Newhoudt-Druchen, alisema kuwa mkalimani huyo alikuwa akifanya mambo yasiyokuwa na maana.
Akizungumzia kuhusu hilo Bruno Druchen alisema: “Lugha za alama si za kuigiza kama wengi wanavyofikiri huku wakishindwa kujua kwamba ni muhimu kwa kuwasaidia watu wasiosikia.”
Kauli hiyo ameitoa kutokana na malalamiko yaliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii na kundi kubwa la watu wenye tatizo la kusikia vizuri.
Druchen alisema kuwa shirikisho lake limewahi kulalamika kwa kufanyiwa tukio kama hilo mwaka jana kwenye sherehe za chama cha ANC ambako Rais Jacob Zuma alihudhuria.
Wakati hayo yakijili maelfu ya watu nchini humo wameendelea kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Nelson Mandela aliyefariki Alhamisi ya wiki iliyopita jijini hapa.
Tayari maelfu ya waombolezaji walishiriki kutoa salamu zao za mwisho kwa mwili huo kuanzia juzi sambamba na familia ya Mandela ambao kwa pamoja walizunguka jeneza la wazi la kinara huyo wa kuzuia ubaguzi wa rangi kuashiria kuanza rasmi kwa siku tatu za utoaji wa heshima za mwisho.
Bado kumekuwapo na misururu mirefu kuelekea Ikulu ya nchi hiyo mjini Pretoria, ambako mwili wa kiongozi huyo umewekwa kwa muda wa siku tatu.
Wakati wananchi wa Afrika Kusini wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Nelson Mandela mjini Pretoria, raia wa kigeni nao wameendelea kufurika nchini humo kutoa heshima zao kwa mwili wa Mandela huku wakimlilia na kusema aliwaunganisha na wakati mwingine kuwapatia uraia licha ya kuwa walitoka nje ya Afrika Kusini.
Vyumba vyapanda Qunu
Ikiwa inatarajiwa Mandela kuzikwa Desemba 15, vyumba vya wageni nchini hapa vimepanda kutoka randi 200 kwa siku hadi kufikia randi 500 kwa usiku mmoja.
Akizungumzia kuhusu hilo Ntomboxolo Mazwi, alisema kuwa ametakiwa kulipa randi 500 kwa usiku mmoja hadi kufikia randi 600.

TANZANIA DAIMA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top