Akizungumza na Tanzania Daima, Jaji Mutungi alisema kuwa ameyapokea malalamiko hayo na kwa sasa anajiandaa kuanza kuyafanyia kazi.
Jaji Mutungi alisema kuwa suala hilo litafanyiwa kazi haraka na atahakikisha kutoa majibu hayo ndani ya kipindi kifupi.
“Ni kweli ofisi yangu imepokea barua hiyo na kwa sasa najielekeza kuanza kuyatekeleza na ninaahidi kumaliza utekelezaji kwa haraka na kisha kutoa mwongozo wa suala hilo.
Alisema kuwa hawezi kuweka wazi ni muda gani suala hilo litachukua lakini alisisitiza kuwa utekelezaji wake utakuwa ni mfupi kutokana na uzito wa suala hilo.
“Inaweza kuchukua wiki moja, mbili au hata tatu lakini kikubwa ni kuhakikisha tunayafanyia kazi yale yote yaliyowasilishwa katika meza yetu tena kwa haraka sana,” alisema.
Mwigamba aliomba mwongozo huo ujikite kwenye kipengele kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume na utaratibu.
Alisema Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2004 kipengele 5.3.2 (c) kinasema kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi moja.
Alibainisha kuwa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 kipengele cha 6.3.2 ( c) inayozungumzia muda wa uongozi inasomeka kuwa kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena, mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi, huku akibainisha kuwa sentensi kuhusu ukomo wa uongozi imeondolewa.
Alisema sio kweli kwamba CHADEMA haijawahi kuwa na katiba ambayo ina ukomo wa uongozi, na kwamba katiba ya 2006 haikuandikwa upya bali marekebisho yalifanywa kwa baadhi ya vipengele huku kipengele 5.3.2 (c ) kikiwa hakijawahi kujadiliwa
TANZANIA DAIMA
Post a Comment