RAIS wa zamani wa Afrika Kusin, Nelson Rolihlahla Mandela ‘Mzee Madiba’ alikuwa kipenzi cha wengi mashuhuri duniani na baadhi yao walipokuwa wakitangulia mbele ya haki yeye alijua zamu yake itafika.
Mandela alishajiandaa kwa kifo tangu mwaka 1964 alipotoa hotuba ya ukombozi na kusema wazi kwamba alikuwa tayari kufa kwa ajili ya kupigania demokrasia ya nchini yake.
Maneno hayo aliyarudia tena April 20, 2011 akisisitiza kwamba hakuwa akikiogopa kifo kama walivyo wengine na alijua siku moja atakufa na kuwa tayari kwa tukio hilo.
Kwa maana hiyo, hata baadhi ya watu maarufu aliopata kupiga nao picha walipotangulia kwa miaka tofauti, Mzee Madiba alijua kwamba zamu yake ilikuwa ikikaribia.
Baadhi ya viongozi na watu maarufu aliowahi kupiga nao picha na wakamtangulia ni pamoja na Rais wa Kwanza wa Tanzania, hayati Julius Nyerere (alifariki dunia Oktoba 14,1999).
Wengine ni mwanamuziki maarufu duniani, Michael Jackson (alifariki dunia Juni 25, 2009), aliyekuwa Kiongozi wa Wapalestina, Yasser Arafat (alifariki dunia Novemba 11, 2004), Muammar Gaddafi aliyekuwa Rais wa Libya (aliuawa na waasi Oktoba 20, 2011) na mwanamuziki wa Marekani, Whitney Houston (alifariki dunia Februari 11, 2012).
GPL
Post a Comment