Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Fedha na Uchumi, Deos
Filikunjombe amesema mkakati ya kuwang’oa mawaziri wanaoshindwa
kutekeleza mipango ya Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi ni
endelevu.
Filikunjombe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Ludewa, Njombe alitoa msimamo huo wakati wa Ibada ya Sikukuu ya Krismasi
iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu William Pasvual
Johson lililopo Kijiji cha Ilela, Kata ya Manda wilayani hapo.
Alisema mkakati wa wabunge kuwawajibisha mawaziri
wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao hauna nia mbaya, bali unalenga
kuhakikisha mawaziri na Serikali wanatekeleza majukumu yao.
“Siyo kwamba wabunge tunakuwa wakali, kimsingi
tunatimiza wajibu wetu tunachotaka sisi, mawaziri na Serikali watimize
wajibu wao,” alisesma.
Filikunjombe alisema tukio la hivi karibuni la
wabunge kushinikiza mawaziri waliozembea katika Operesheni Tokomeza
Ujangili lilifanyika kwa nia ya kuwatetea wananchi.
Alisisitiza kuwa hata kesho ikitokea kuna waziri
ambaye anazembea kutekeleza majukumu yake, wabunge hawatasita
kushughulika naye.
Akitoa salamu za Krismasi na Mwaka Mpya, Padri wa
kanisa hilo, Reuben Ngoye alimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi wa
busara wa kuwang’oa mawaziri ambao walililalamikiwa na wabunge kwa
kushindwa kusimamia vizuri utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
“Uamuzi wa Kikwete wa kuwaengua mawaziri hao umenifanya niamini kuwa kiongozi wetu ana msimamo,” alisema Padri Ngoye.
MWANANCHI
MWANANCHI
Post a Comment