Muigizaji
wa vichekesho kwenye kundi la Mizengwe Hemedi Khalida maarufu kama
Mkwere ameangukiwa na neema ya ubalozi wa kuhamasisha upatikanaji wa
jina la kampuni ya simu iliyoziduliwa bila jina. Kampeni hiyo
itafanyika kupitia simu na mitandao mbalimbali ambapo wananchi
wanatakiwa kuipatia jina kampuni hiyo. Mbali na hayo Mkwere atapata
nafasi ya kupita mitaa mbalimbali akiwahimiza wananchi kupiga kura.
Sekta
ya mawasiliano ya simu Tanzania na Afrika Mashariki imepata matumaini
mapya kufuatia kuingia kwa kampuni mpya ya simu ya kipekee, ya ubunifu,
yenye kuamini jamii, na yenye ushindani kuliko zote, kuzinduliwa bila
jina.
Pamoja
na ahadi yake ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mawasiliano ya mtandao
wa simu, kampuni hiyo mpya kwa wakati mmoja imezindua pia kampeni ya
kiubunifu inayotambulika kwa jina la “Tupe Jina” itakayofanyika kwa njia
ya mtandao na ujumbe mfupi katika simu kwa lengo la kuipa fursa Afrika
Mashariki kuichagulia jina bora kampuni hii kwa kupiga kura.
Hii
ni kampuni ya kwanza ya simu Afrika Mashariki ambayo kweli inajali na
haigopi kuamini watu, na hakuna kampuni nyingine inaweza kuthubutu
kufanya hivyo. Hakuna kampuni yoyote duniani iliyoweza kuzinduliwa bila
jina na kutoa jukwaa kwa kampeni ya kusisimua kabla ya jina kuwekwa
hadharani.
“Tupe
Jina” ni kampeni itafanyika kwa awamu mbili katika mtandao, ujumbe wa
simu na mtandao wa kijamii wa facebook. Katika awamu ya kwanza, Afrika
Mashariki inapaswa kuteua majina ambayo wanapenda hii kampuni mpya
iitwe.
Mshirki
anaweza kuchagua jina kwa kuingia katika mtandao wa Unaweza kuteua jina
kwa njia ya magogo kwenye mtandao wa www.giveusaname.net au kutuma
ujumbe wa simu ukiambatanishwa na jina analopendekeza kwenda namba
15678 au aingie katika mtandao wa www.facebook.com/giveusaname. Katika
awamu ya pili ya kampeni, jopo litatathmini majina yote na itatoa majina
matano ambayo yamependekezwa mara nyingi zaidi, ya kipekee na yenye
ubunifu.
Baada
ya hapo Afrika Mashariki watapiga kura kwa ajili ya kupata jina bora
moja ambalo hatimaye litakuwa jina la kwanza la kampuni hii ya
mawasiliano ya simu ambayo daima itakuwa ya kwanza ya Kiafrika
Mashariki. Mshindi katika kampeni hii, mtu ambaye atakuwa amechagua jina
ambalo hatimaye litakuwa la kampuni atajishindia muda wa bure wa kupiga
simu za ndani na SMS bure kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Zawadi
zingine zitakuwa simu za kisasa za ‘smartphone’ na kompyuta za
kiganjani (tablets) kwa washiriki wa kampeni hii ya “Tupe Jina”.
Kutokana
na wataalam kutabiri kuongezeka kwa pato la taifa la Tanzania kutoka
asilimia 4 hivi sasa hadi asilimia 7 mwaka 2015, sekta ya mawasiliano
ina nafasi kubwa ya katika ukuaji wa uchumi katika miaka ijayo na
kampuni hii mpya ya mawasiliano ya inawakilisha sura ya kasi hii kubwa
ya ukuaji.
Tanzania
inabaki kuwa ni moja ya nchi zenye kiwango cha kuingiza simu chini ya
asilimia 50 kufikia Juni 2013, jumla ya matumizi ya mawasiliano ya simu
nchini humo ni chini ya wastani kwa nchi za Afrika.
Hii
kampuni mpya ya simu kwa umuhimu mkubwa itawekeza kiasi kikubwa cha
fedha kutoka kwa wateja wake kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu kwa
watu wa Tanzania katika sekta ya afya na hasa katika tiba za kimtandao
na vituo vya elimu ya masafa.
Hii
tafsiri yake ni kwamba kuwekeza idadi kubwa ya faida katika kuwezesha
Afrika Mpya kuzingatia ongezeko la watumiaji wa mawasiliano ya simu, na
zawadi bora ambayo kampuni hii inatarajia katika miaka ijayo ni kukuza
sekta ya afya.
Baada
ya kampeni ya “Tupe Jina” wananchi wa Tanzania watapata nafasi ya
kupeleka namba zao wanazopendekeza kabla ya kutangazwa na kuwekwa
hadharani kwa jina la kampuni.
Post a Comment