Kwa mujibu wa ratiba ya ziara ya Dr. Slaa iliyotolewa tarehe 3 disemba ni kwamba leo tarehe 5 Dr. Slaa anatakiwa kuwa Kakonko...
Kakonko ni jina la makao makuu ya Wilaya ya Kakonko katika Mkoa wa Kigoma.
Taarifa
tulizozipata zinaarifu kuwa, msafara huo umegonga kisiki baada
ya wananchi kuvizunguka viwanja vya bunge ambako mkutano huo
unafanyika huku wakiwa na fimbo na mawe....
Majira ya saa tisa na dakika kadhaa, gari ya M4C yenye vijana watatu ndani yake ilionekana ikiwazunguka wananchi hao huku ikiwatishia kuwakamata endapo wataleta fujo eneo hilo.
Baadaye
mkutano huu unaonekana kuanza huku Dr. Slaa akiwa chini ya
ulinzi mkali wa vijana 15 wa Redbrigedi na polisi kadhaa
waliojihami....
Baada
ya mkutano kuanza salam za Dr. Slaa zilipokelewa kwa matusi
na sauti za kuzomea zikisikia kumtaka Zitto Kabwe ambapo Slaa
aliwatuliza kwa kuwambia kuwa atawaeleza mwishoni alipo Zitto
Kabwe...
Dakika
kadhaa baada ya mkutano kuanza, kijana mmoja anaonekana kutiwa
mbaroni na vijana wa Redbrigedi kwa tuhuma za kupiga picha
kwa kutumia simu yake bila ridhaa yao huku wakimtaka aonyeshe
vitambulisho vyake kama kweli ni mwandishi wa habari...
Kwa mujibu wa mitandao mingine, uongozi wa CHADEMA majira ya saa tisa umepingwa vikali na watanzania wenye uchu wa kujua hatima ya sekeseke hili baada ya kutundika picha mbili za mwaka 2010 wakidai kuwa ni za leo katika mkutano wa Dr. Slaa.....
Kwa mujibu wa mitandao mingine, uongozi wa CHADEMA majira ya saa tisa umepingwa vikali na watanzania wenye uchu wa kujua hatima ya sekeseke hili baada ya kutundika picha mbili za mwaka 2010 wakidai kuwa ni za leo katika mkutano wa Dr. Slaa.....
1 comments:
1. Watanzania tumeapa kuitokomeza ccm hata kama ccm wataendelea kuhujumu mikutano ya chadema. CCM endeleeni kuvuruga amani katika mikutano ya chadema lakini mjue kwamba Hatuko tayari kuendelea kutawaliwa na Wezi/Walanguzi/Majangili/Majambazi/Wauaji/watesaji/Mafisadi. Maana halisi ya ufisadi ni Wezi/Walanguzi/Majangili/Majambazi/Wauaji/watesaji/Mafisadi hivyo ccm msizani maovu yenu kuyaita ufisadi maana yake hatujui
ReplyPost a Comment