Mbunge wa
Temeke, ambaye pia ni Mlezi wa timu ya netiboli ya Temeke Queens, Abbas Mtemvu,
akimrejeshea Kombo la ubingwa Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania
(CHANETA), Anna Kibira lililokuwa linashikiliwa na mabingwa watetezi wa michuano
ya Taifa Cup, Temeke Queens. Hafla hiyo ilifanyika wakati wa ufunguzi wa
michuano hiyo kwenye Uwanjawa Taifa Dar es Salaam.
Mtemvu
akimkabidhi kocha wa Temeke Queens, Amina Mussa fedha kwa ajili ya posho za
wachezaji na viongozi wa timu hiyo inayoshiriki michuano hiyo.
Mwanaidi Ngubege wa
Temeke Queens (kushoto) akijiandaa kufunga goli dhidi ya timu ya Mkoa wa
Katavi.
Lillian
Sylidion wa Temeke akidaka mpira
Mchezaji
Sekela Dominick (kushoto) wa timu ya Temeke Queens akigombea mpira wa juu ya
Rose Israel wa timu ya Mkoa wa Katavi katika mashindano ya kuwania Kombe la
Taifa (Taifa Cup) siku ya ufunguzi wa michuano ya mchezo wa netiboli, kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Temeke Queens ilishinda 58-27. (PICHA NA RICHARD
MWAIKENDA)
Benchi la
wachezaji wa timu ya Mkoa wa Katavi
Kocha
Amina Mussa wa Temeke akitoa mawaidha kwa wachezaji wakati wa
mapumziko
Post a Comment