Baba huyo ambae
anajulikana kama Mr Tafadzwa Kachere na mwanae Tapiwa walijeruhiwa vibaya na
mamba huyo hapo jana na kupelekea wao kulazwa katika hospitali ya
Chitungwiza.
Tapiwa alijeruhiwa kiasi
cha mguu wake wa kushoto kukatwa, wakati mkono wa kushoto wa Baba yake uliumizwa
vibaya, Mr Kachere alisema kuwa mamba huyo aliwashambulia wakati watoka katika
bustani yake kuelekea nyumbani, Mzee huyo aliendelea kusema kuwa walipokuwa
wanavuka mto huo kijana wake akiwa nyuma alisikia mwanae akipiga mayowe ya
kuomba msaada na ndipo alipoamua kwenda na kupambana na mamba huyo ili aweze
kumuokoa mwanae aliyekua anaangaika baada ya kung'atwa mguu
wake.
Mzee huyo aliendelea
kusema " niliangaika kufungua mdomo wa mamba huyo kwamikono yangu lakini
ilishindikana, pamoja na kumchoma choma na mianzi mdomoni lakin ilikuwa ni ngumu
mno kumwachia mwanangu na ndipo nilipomchoma mamba huyo na mwanzi machoni nikiwa
nimekaa mgongoni mwake na kumwachia mwanangu na yeye kuangaika katika maji na
mimi nikambeba mwanagu mgongoni taratibu tukajikokota kutoka nje ya
mto.
Baada ya shambulio hilo
tulipata msaada wa kwanza katika hospitali ya Nyadire kabla ya kupelekwa
hospitali ya kati 'Chitungwiza"SOMA ZAIDI
Mr Kachere ametoa wito
wa msaada wa kununua mguu wa bandia kwa ajili ya mwanae. Kachere alisema "Naomba
msaada kwa yeyote mwenye uwezo ili ninunue mguu wa mwanangu kwani yeye bado
anahitaji kwenda shule na hadi sasa yeye anaamini kuwa mguu wake
utarudi.
Si uongo yeye anaamini
kuwa mguu wake umeondolewa kwa madhumuni ya matibabu na sijui ni jinsi gani
nitamfikishia taarifa ya mguu wake, alimalizia kusema Baba huyo kwa uchungu na
kulia.
Hii ni kwababa mwenye
upendo wa dhati kufa kwaajili ya mwane Je ingekuwa wewe
ungefanyaje....?
on Sunday, December 29, 2013
Post a Comment