MKASA MZIMA
ULIKUWA HIVI.....
Mwanamke
mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mke wa mtu anateseka hospitalini baada ya
kuchomwa na mafuta ya kupikia ya moto na ndugu yake baada ya kuhisiwa kuiba
vocha ya simu ya mtandao wa Telecel yenye thaman ya senti 50 huko
Zimbabwe.Kijana huyo aliyejulikana kwa
jina la Otilia Kosa anayeishi Plot 16, Tsungwizi Ridge maeneo ya Nyazura huko
nchini Zimbabwe anateseka katika hospitali ya Rusape General Hospital akiuguza
majeraha aliyoyapata baada ya kumwagiwa mafuta ya moto na ndugu yake.
Inadaiwa kwamba mnamo
tarehe 27 Decemba 2013, Otilia alimuuliza ndugu yake Kudakwashe kama yeye ndiye
aliyetumia vocha yake ya mtandao wa Telecel yenye thamani ya senti 50 za
kizimbabwe.Kudakwashe alikataa kuwa hakutumia vocha hiyo na hapo ndipo mtafaruku
mkubwa ulipotokea kati ya wawili hao.
Cha kushangaza ,siku
iliyofuata kikao cha familia kilikaa ili kuwapatanisha wawili hao ambao
walishindwa kuelewana na mpaka kufikia hatua mbaya ambayo ingepelekea kuvunja
udugu wao.Hata hivyo, wanafamilia hao walishindwa kuwapatanisha ndugu hao na
hivyo kuongeza mpasuko kati yao.
Ilidaiwa kuwa baada
ya kukosa muafaka huo,Kudakwashe alipatwa na hasira kali iliyompelekea yeye
kuingia jikoni na kuchemsha mafuta ya kupikia na kummwagia nduguye huyo (Otilia)
katika maeneo ya uso,shingo,kifua,mikono na
tumboni.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Afisa wa Polisi wa ZRP Nyazura, Inspekta hikima Sanida
alinukuliwa akisema "We have arrested the suspect and recorded a warned and
cautioned statement in which she admitted scalding the victim with hot cooking
oil. She was charged with first-degree assault and criminal violation of the
Domestic Violence Act,"
Post a Comment