Samahani kwa muonekano wa
picha ila ndio hali halisi Kiteto
Mauaji yakutisha
Kiteto
·
-- Wakulima wavamiwa,
wachinjwa
· -Risasi za moto zatumika
· -Wachomewa nyumba zao
· -RC Manyara awasili kuwapa
pole
Na Mohamed
Hamad
WILAYA ya Kiteto imeingia
kwenye orodha ya maeneo yanayotisha kwa mauaji ya kinyama baada ya wakulima
kuuawa mara kwa mara na wafugaji kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za
kugombea ardhi
Miongoni mwa waliouawa
kinyama Dec 20 kwa kuchinjwa shingo yake ni Juma Mlagwa (49) wa Kitongoji cha
Kalikala Kata ya Njoro (Kiteto) ambaye alivamiwa nyumbani kwake usiku na kundi
la vijana wa kifugaji masai (makorianga)
Imeelezwa kuwa wakati
anavamiwa zilisikika Risasi zikipigwa juu Kitongojini hapo na baada ya watu
kuendelea kujificha ndani vijana hao walianza kunyinyizia nyumba zao mafuta aina
ya petrol kisha kuwasha moto
Akizungumza mbele ya Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Ally Mussa Mwenyekiti wa Kitongoji hicho alisema siku hiyo
haitasahaulika mashani mwake kwa yaliyotokea kutokana na vitendo hivyo akisema
ilikuwa mara ya kwanza kuona mtu anachinjwa hadharani
“Nilichomewa Pikipiki zangu
mbili pamoja na vitu mbalimbali vya ndani zikiwemo nguo vyakula, lakini
nilichonusuri ni roho yangu ambayo hadi leo nasema najivunia uhai nilio
nao”alisema Mwenyekiti huyo
Alisema chanzo cha mauaji
hayo ni jamii ya kifugaji wamasai kuingiza mifugo yao kwenye shamba la mmoja wa
wakulima Kitongojini hapo na baada ya kukatazwa walimpiga kisha nae kupigwa
ndipo wakakusanyana kupanga uvamizi huo CHANZO MATUKIO
BLOG
Hata hivyo baada ya
kufikishwa taarifa kwa viongozi wa Serikali walidaiwa kulifika Kitongojini
lakini walikataa kwenda kuongea nao km chache kwa madai kuwa ni uongo kwamba
hakuna watu waliokusanyana
Akielezea hayo Mwenyekiti
huyo alisema tatizo ni uongozi dhaifu kuanzia ngazi ya Kitongoji hadi Wilaya
ambapo alidai kuwa ukabila umeshamiri kwa viongozi kujiona kuwa wanahaki ya
kutfanya utetezi katika upande mmoja
Kwa upande wake Lairumbe
Mollel Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya akizungumzia sakata hilo
alimzodoa mwenyekiti huyo wa Kitongonji kuwa ni muongo kwani baada ya wao kufika
kabla ya tukio alikataa kuwataja wahusika
Hata hivyo kauli hiyo
ilionekana kutokuwa na mashiko baada ya mwenyekiti huyo wa Kitongoji kuonyesha
udhaifu wa viongozi hao akisema baada tu ya kufika hawakuweza hata kukubali
kupelekwa walikoweka kambi vijana hao wa kimasai
“Baada ya kufika walitaka
nisema majina ya walioleta fujo na nilipowataka twende eneo la tukio wakakata
nakuona kuwa hawakuwa na njia njema kisha wakarejea Kiteto ambapo usiku vijana
hao wakatekeleza azima yao ya kuchinja mtu mmoja na kumpiga mwingine risasi
kisha kuwajeruhi watu saba”alisema Mwenyekiti huyo wa
kitongoji
Waliofariki katika uvamizi
huo ni pamoja na Juma Malagwa (49) ambaye alichinjwa shingo, Yohana Ivo (33)
ambaye alipigwa sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kifo pamoja na watu
wengine saba kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa kujeruhiwa kwa
fimbo na mapanga
Waliolazwa katika Hospitali
ya Wilaya ya Kiteto ni Hoti Daniel (38) Emanuel matias (21) Juma Bahati (13)
Mwajuma Hamisi (20) Habiba Ally (16) Mwajuma Martin pamoja na Musa Juma (16)
aliyepelekwa Dodoma kwaajili ya matibabu
Hata hivyo mkuu huyo wa
Mkoa wa Manyara Elaston Mbwillo akiwa katika kitongoji hicho aliwapa siku 30
viongozi wa Wilaya ya Kiteto kuweka utaratibu wa kuwatambua wananchi hao ili
kuondoa tofauti zao waweze kufanya kazi bila bughdha
“Ninyi wananchi mwende
kujisajili Kijijijini ili Serikali iwatambue kwani maisha bora kwa wananchi
yatapatikana kwa kufahamika mlipo ili mpatiwe huduma za jamiiambazo kwa sasa
hamna hata moja”alisema Mbwillo
Mwisho..CHANZO http://lindegeimfor.blogspot.com
Post a Comment