ZIKIWA zimesalia siku 15 kukatika kwa mwaka 2013 na kuukaribisha 2014, Ijumaa Wikienda linakuletea matukio kibao yaliyotafsiriwa kuwa ni nuksi katika ulimwengu wa mastaa Bongo.
BONGO MOVIES
Katika kipindi chote hicho, tasnia ya filamu (Bongo Movies) ilipata pigo zaidi ya mara kumi baada ya kuondokewa na mastaa wake tangu mwaka huo ulipoanza alipofariki dunia Juma Kilowoko ‘Sajuki’. Ilikuwa mapema Januari 2.
Kama hilo halitoshi, baadaye ilipata tena mapigo ya kuwapoteza waigizaji wake mahiri kama Jaji Khamis ‘Kashi’ na Zuhura Maftah ‘Melisa’.
Pia baadhi ya mastaa wakubwa walipata misiba ya wazazi, watoto, rafiki au ndugu. Aliyefiwa na mwanaye ni Steve Nyerere. Aliyefiwa na baba ni Wema Sepetu. Aliyefiwa na mume ni Wastara Juma.
Mbali na vifo, tasnia hiyo ilipata misala kibao ikiwemo mastaa wake kuwekwa nyuma ya nondo za polisi na mahakamani kama Wema na Kajala ambaye alihukumiwa jela lakini Wema akamlipia faini ya Sh. milioni 13.
Aunt Ezekiel yeye alikwenda polisi kuripoti baada ya kupigwa chupa akiwa klabu.
Kwa upande wake Wolper aliingia mkenge na kuukabidhi moyo wake kwa mwanaume, Dallas aliyedai kumtenda kimapenzi.
Hata hivyo, kubwa zaidi kwa tasnia hiyo ni kuanguka kwa soko la filamu kwani hakuna aliyefanikiwa kuvunja rekodi ya marehemu Steven Kanumba aliyefariki Aprili 7, 2012.
Marehemu Albert Mangweha 'Ngwair'.
BONGO FLEVAKwenye Bongo Fleva, nako hali haikuwa shwari kwa kuwa ilikuwa ukiisha msala huu unaibuka mwingine huku kubwa likiwa ni vifo vya mastaa wawili wakubwa.
Aliyeanza kutangulia mbele ya haki ni Alberth Mangweha ‘Ngwea’ aliyefariki dunia Mei 28, mwaka huu huko Sauzi. Alifuatiwa na rapa mwenzake, Langa Kileo aliyefariki dunia Juni 13.
Misala haikuishia hapo kwani katika kipindi cha mwaka 2013, wasanii wengi waliandamwa na skendo ya matumizi na kusafirisha madawa ya kulevya.
Katika msala huo, mastaa kibao walijikuta matatani. Agness Gerald ‘Masogange’ na mwenzake Melisa Edward walinaswa Sauzi huku Sandra Khan ‘Binti Kiziwi’ akifungwa nchini China.
Baadhi ya mastaa walijitokeza na kukiri kutumia madawa ya kulevya huku wakiapa kuwa wameacha. Mifano ni mingi, wapo Ray C, Q-Chillah, Chidi Benzi na Ibra Da Husler aliyekuwa memba wa Nako 2 Nako Soldiers.
Wengine waliotuhumiwa lakini wamekuwa wakikataa kujihusisha na unga ni pamoja na TID na Lord Eyez.
Achilia mbali unga, bifu zilikuwa za kumwaga. Diamond aliongoza kwa kutuhumiwa kwa wizi wa nyimbo huku akijiwekea bifu na wasanii kama Bob Junior, Q-Chillah, H. Baba, Baba Levo, Dayna na wengine kibao.
Kwa upande wake Chidi Benz alijikuta akikorofishana na Kalapina kabla ya baadaye kuvaana na Kassim Mganga. Yeye alituhumiwa kutumia unga, naye akamtuhumu mwenzake kwa ushirikina.
Pia kulitokea mpasuko mkubwa kati ya wasanii hao baada ya kuwepo makundi mawili, moja likipinga unyonyaji wa wasanii huku lingine likiona ‘poa tu’.
WAGONJWA
Katika kipindi hicho, mastaa wengi waliripotiwa kuwa wagonjwa kama Aunt Ezekiel, Lady Jaydee, Amanda, Otilia, Wema, Diamond, Sara Mvungi, Wastara Juma, Wolper, Idrissa Kupa, Steve Nyerere na Shija. Kweli 2013 ilikuwa majanga!
Kuhusu uchambuzi mwingine wa dansi, taarab, komedi na nyanja nyinge fuatilia magazeti yajayo ya Global Publishers.
GPL
Post a Comment