Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla akiingia ukumbini kwa ajili ya
kufungua Kongamano la Viongozi wa Michezo Wanawake Barani Afrika
lililofanyika katika Hoteli ya Peacok jana Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel
(aliyesimama) akimkaribisha Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Mhe. Amos Makalla (Kulia) wakati wa Kongamano la Viongozi wa
Michezo Wanawake lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu
wa Mfuko wa Anita Foundation Dr. Anita White.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla akifungua Kongamano la Viongozi
wa Michezo Wanawake lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Washiriki kutoka nchi mbalimbali
wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa katika kongamano
hilo jana Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars. Wa kwanza
kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, anayefuata kushoto ni Mkuu wa Mfuko wa Anita Foundation Dr.
Anita White, kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard
Thadeo, na anayefuata kulia ni Mkurugenzi wa Sera, Shirika la Right to
Play Afrika Bw.Denis Bright, waliosimama nyuma ni wachezaji wa Twiga
Stars ambao pia wameshiriki katika Kongamano la Viongozi wa Michezo
Wanawake lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment