Mkurugenzi Mkuu
wa TFDA, Hiiti B. Sillo akikabidhi tozo maalum kwa Mkurugenzi wa USAID
Bi. Sharon L. Cromer katika hafla iliyofanyika TFDA makao Makuu.
Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti ya TFDA na ujumbe wa USAID wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo akiuonesha ujumbe wa USAID moja ya vitabu rejea vya viwango vinavyotumika katika maabara ya TFDA.
Mkurugenzi
Mkazi wa USAID, Sharon L. Cromer ameahidi kuendelea kushirikiana na
TFDA katika kuhakikisha afya ya wananchi inalindwa kwa kuisaidia Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) katika kuijengea uwezo kwenye masuala ya
udhibiti wa usalama na ubora wa bidhaa za
chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba nchini.
chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba nchini.
Kauli
hiyo imetolewa leo tarehe 17/12/2013 katika ziara ya ujumbe wa USAID
iliyofanyika Makao Makuu ya TFDA kwa lengo la kujionea ufanisi wa
utendaji wa Mamlaka kufuatia misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa
na Shirika hilo la kimaendeleo kwa TFDA kuanzia mwaka
2011 hadi sasa.
2011 hadi sasa.
USAID
imekuwa ikiisaidia TFDA katika kuwajengea uwezo watumishi wake hususan
udhamini wa mafunzo kwa wakaguzi wa dawa, mafunzo kwa watumishi kuhusu
mifumo bora ya utendaji kazi na utoaji huduma pamoja na manunuzi ya
vifaa vya maabara ya Mikrobiolojia kwa lengo la kuendelea
kukidhi vigezo vya Shirika la Afya Duniani (WHO).
kukidhi vigezo vya Shirika la Afya Duniani (WHO).
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo, alikabidhi tuzo maalum kwa
shirika la USAID ikiwa ni alama ya kutambua mchango wa USAID katika
mafanikio yaliyofikiwa na Mamlaka kwa kipindi cha miaka 10 (2003-2013)
Post a Comment