|
Bwana harusi akiwa na mpambe wake kanisani wakimsubiri bibi Harusi |
|
Jamaa wameshika vichwa hali haieleweki |
|
Bi Harusi Naomi Ngoje akiwa amejilalia chumbani akiwa anahuzunika na kushangaa wazazi wake kurudisha mahali ya mchumba wake
HABARI zilizotufikia hivi punde kutoka nyumbani kwa familia ya Bi
harusi ambayo ilikuwa ikipinga ndoa isifungwe kutokana na Bwana harusi
kushindwa kumalizia sehemu ya Mahari zinadai kuwa ndoa imevunjwa rasmi na kilichobaki
ni mzozo wa kurudishiana fedha.
Pande hizo mbili ya Kiume na Kike zimengia kwenye Mzozo na kuvutana
kuhusu fedha baada ya Wazazi wa Mwanamke kukubali kurudisha fedha hizo pamoja
na vitu walivyopokea huku kikubwa kikiwa ni upande wa Mwanaume kudai wapewe
papo hapo.
Vitu vinavyodaiwa ni Fedha taslimu takribani Shilingi 310,000/= ambazo
zilitolewa kwa ajili ya Mkaja pamoja na kiingilio, Blanketi na Mashuka.
Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mtandao wako kila wakati unaokupa
habari zisizoacha shaka kwa msomaji.
NaMbeya yetu
|
on Sunday, December 29, 2013
Post a Comment