Pia imeyaagiza makundi hayo kuzingatia sifa
zilizotajwa kwenye Sheria ya Marekebisho ya Katiba wakati wa uteuzi wa
majina ya watu watakaowapendekeza.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa
Sheria na Katiba, Mathias Chikawe alisema kuwa makundi hayo yanatakiwa
kuwasilisha kwa Rais orodha ya majina ya watu wasiopungua wanne na
wasiozidi tisa.
“Rais Jakaya Kikwete Desemba 13, 2013 alitoa
tangazo kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2A) cha kifungu cha 22 cha
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 alialika kila kundi kutoka
pande zote za Muungano kuwasilisha kwake majina kwa ajili ya kuzingatiwa
kwenye uteuzi,” alisema Chikawe.
Alibainisha kuwa kila kundi linatakiwa kuzingatia
umri, jinsia, uzoefu, sifa na sehemu ya makazi ya mtu aliyependekezwa.
Jumla ya idadi ya wajumbe kutoka Zanzibar hawatapungua moja ya tatu ya
wajumbe wote.Kwa habari zaidi bofya na Endelea.......
Post a Comment