Na GLADNESS MUSHI , Arusha
KAMPUNI ya Smile ya mawasiliano ya Smile imeweka mikakati ya kusaidia shule za Serikali ambazo zina maabara kwa kutoa huduma ya
mawasiliano(internet)bure itakayowawezesha wanafunzi waweze kusoma kwa kupitia mitandao.
KAMPUNI ya Smile ya mawasiliano ya Smile imeweka mikakati ya kusaidia shule za Serikali ambazo zina maabara kwa kutoa huduma ya
mawasiliano(internet)bure itakayowawezesha wanafunzi waweze kusoma kwa kupitia mitandao.
Hayo
yameelezwa na Deo Ndejembe ambaye ni meneja kitengo cha mauzo katika
kampuni hiyo wakati akiongea kwenye uzinduzi wa mtandao wa smile kwa
mkoa wa Arusha mapema leo.
Deo
alisema kuwampango huo unalenga kuimarisha huduma za maabara katika
shule za sekondari za serikali kwani wanafunzi wakiwa na huduma hizo
wataweza kusoma na kwenda pamoja na soko la dunia ambalo linategemea
zaidi huduma za mitandao.
Alidai
kuwa mpango huo utaweza kuwanufaisha zaidi shule ambazo zina maabara
pamoja na kompyuta hivyo basi hata kwa shule ambazo hazina maabara
zinatakiwa kuweka mara moja ili ziweze kunufaika na mpango huo ambao
umeshaanza
“Tunataka
kuona kuwa lile lengo la serikali ambalo lililenga shule ziwe na
maabara linatimia lakini pia maabara ziwe za kisasa zaidi na
ziweze kupata teknolojia ya mawasiliano bure kwani itasaidia hata ufaulu wa masomo kama sayansi kuweza kuongezeka’alisisitiza Deo
ziweze kupata teknolojia ya mawasiliano bure kwani itasaidia hata ufaulu wa masomo kama sayansi kuweza kuongezeka’alisisitiza Deo
Wakati
huo huo alidai kuwa mpango huo wa kutoa huduma za Tekonlojia umeshaanza
kwa shule 10 ndani ya Jiji la Dar es saalam lakini kwa mkoa wa Arusha
shule ya Arusha School tayari imeshanufaika na mpango huo ambao ni bure
Naye
Afisa mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)Innocent
Mongi alidai kuwa bado mkoa wa arusha unahitaji huduma za mawasiliano
zaidi kutokana na mwingiliano wa huduma kama vile uchumi, na utalii.
Mongi
alidai kuwa uwepo wa mtandao huo wa Smile kwa mkoa wa arusha
pia utachangia wafanyabiashara wakubwa na wadogo kuweza kufanya
biashra kutoka katika masoko mbalimbali duniani .
“Napenda
kuwasihi wakazi wa Arusha kuhakikisha kuwa wanatumia vema mtandao huo
ili kuraisisha shuguli mbalimbali za maendeleo kwa mkoa wa arusha na
kutokana na hili tunaamini kuwa Arusha itapata
mabadiliko makubwa”alisema Mongi
Post a Comment