“PRESS RELEASE” TAREHE 16.12. 2013.
WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 15.12.2013 MAJIRA YA SAA 08:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
ITEGE, KIJIJI CHA ITINDI, KATA YA GALULA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA, NYESI D/O MPONJA, MIAKA 25, MSAFWA, MKULIMA,
MKAZI WA KIJIJI CHA ITINDI ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPELEKWA KITUO CHA
AFYA MBUYUNI KWA MATIBABU BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA NGUMI,
MATEKE NA UBAO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MUME WAKE NDELE S/O
JULIUS, MIAKA 43, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ITINDI. CHANZO NI
WIVU WA KIMAPENZI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANATOA WITO KWA WANANDOA KUTATUA MIGOGORO YAO YA KIFAMILIA KWA
NJIA YA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 15.12.2013 MAJIRA YA SAA 08:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA
MAKANDANA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA, EDDY S/O MBILINYI,
MIAKA 34, MKINGA, MFANYABIASHARA YA NGUO ZA MITUMBA, MKAZI WA UYOLE
ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. CHANZO NI
BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO NA MAWE
TAREHE 14.12.2013 MAJIRA YA SAA 02:00HRS KATIKA KIJIJI CHA MBEYE-ONE,
KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE, KWA TUHUMA ZA KUVUNJA DUKA USIKU
NA KUIBA NGUO ZA AINA MBALIMBALI MALI YA ZIDI S/O JULIUS. KAIMU KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAO
WAKAMATA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE
DHIDI YAO.
WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUACHA NJIA KUPINDUKA NA KUSABABISHA
KIFO NA MAJERUHI.
MNAMO
TAREHE 15.12.2013 MAJIRA YA SAA 11:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA NEWLAND,
KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA, GARI T.668 CGY/T.702 CGZ AINA YA FAW MALI YA
KAMPUNI YA SILENT ROAD HAULAGE LIKIWA LIMEPAKIA MBOLEA TOKA DSM KUELEKEA
NCHINI MALAWI LIKIENDESHWA NA DEREVA KUDRA S/O RAMADHAN, MIAKA 35,
MLUGURU, MKAZI WA UBUNGO- DSM LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA KISHA
KUSABABISHA KIFO CHA TINGO WA GARI HILO MATHIAS S/O JOEL MWENDA, MIAKA
31, MLUGURU, MKAZI WA CHAMAZI –DSM PIA KUSABABISHA MAJERUHI KWA DEREVA
WA GARI HILO AMBAYE AMELAZWA HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE. CHANZO CHA
AJALI KINACHUNGUZWA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[BARAKAEL MASAKI– ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
on Monday, December 16, 2013
Post a Comment