Mhifadhi
wa Hifadhi ya Taifa Saadani, Ismail Omar, akizungumza na waandishi wa
habari wa Chama cha Habari za Sayansi Tanzania (TASJA), wakati
walipotembelea hifadhi hiyo, mkoani Pwani, wakiwa katika ziara ya
kujifunza kuhusu mazingira na viumbe hai.
……………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, TASJA
VITENDO
vya ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyopo wilaya ya
Bagamoyo Mkoani Pwani vimeendelea kupungua siku hadi siku kutokana na
ushirikiano uliopo baina ya wananchi wa kijiji wa Kijiji cha Saadan.
Kauli
hiyo imetolewa na Mhifadhi ya hifadhi hiyo idara ya ulinzi Ismail Omary
alipokuwa akitoa taarifa kwa wanachama wa Chama cha waandishi wa habari
za sayansi(TASJA) waliotembelea hifadhi hiyo kujifunza masuala
mbalimbali.
Alisema
ikilinganishwa na kipindi cha nyuma, kwa sasa vitendo vya ujangili
hifadhini hapo ikiwemo ya uharibifu wa misitu na uwindaji haramu wa
wanyama, vimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na wananchi kutambua
umuhimu wa hifadhi hiyo yenye ukubwa wa kilomita za mraba 1100.
Katika
ziara hiyo ya mafunzo iliyowezeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO)waandishi hao walijifunza masuala
mbalimbali yanayohusiana na umuhimu wa hifadhi za Taifa, kuzitunza na
kuziendeleza.
Kutokana
na kufanisha mafunzo hayo Mwenyekiti wa TASJA Greyson Mutembei,
aliishukuru UNESCO kwa niaba ya wananchi kwa kuhakikisha wanajenga wigo
mpana kwa wanahabari kuhusu taarifa za mazingira hasa za wanyama na
vioumbe hai.
Post a Comment