“PRESS RELEASE” TAREHE 17.12. 2013.
WILAYA YA MOMBA – UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA .
MNAMO
TAREHE 16.12.2013 MAJIRA YA SAA 19:45HRS HUKO KATIKA ENEO LA SOGEA –
MAKAMBINI, KATA YA TUNDUMA, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA
WA MBEYA, ALPHONCE S/O MWANJELA, MIAKA 36, KYUSA, MFANYABIASHARA YA
KUBADILISHA FEDHA, MKAZI WA SOGEA – MAKAMBINI ALIVAMIWA NA KUNDI LA
WATU WANNE WASIOFAHAMIKA KISHA KUMKATA MAPANGA KICHWANI NA KUMJERUHI KWA
KUMPIGA RISASI MGUU WA KULIA KWA KUTUMIA BUNDUKI IDHANIWAYO KUWA S/GUN
NA KUMPORA PESA TASLIMU TSHS 5,200,000/=, USD 2,300, RAND 10,000 NA
ZAMBIA KWACHA 2,000,000. WATUHUMIWA HAO WALIMVAMIA MHANGA AKIWA UMBALI
WA MITA 50 TOKA NYUMBANI KWAKE WAKATI ANATOKA KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA
KUBADILISHA FEDHA MPAKANI TUNDUMA. MHANGA AMELAZWA KITUO CHA AFYA
TUNDUMA NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI. MSAKO MKALI UNAENDELEA DHIDI YA
WAHUSIKA WA TUKIO HILI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA YA
KUBADILISHA FEDHA WAJIUNGE PAMOJA WAFUNGUE DUKA LA KUBADILISHA FEDHA
AMBALO LITAKUWA LIMESAJILIWA ILI ULINZI UWE RAHISI ILI KUONDOA SUALA LA
KUTEMBEA NA FEDHA KIHOLELA NA KUFANYA WIZI/UPORAJI NA UNYANG’ANYI KUWA
RAHISI. PIA ANATOA WITO KWA WALE WANATAKA KUBADILISHA FEDHA WAENDE
KATIKA TAASISI RASMI ZA KUBADILISHA FEDHA KWA USALAMA ZAIDI KWANI
UWEZEKANO WA KATAPELIWA NI MDOGO. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA YA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE
WILAYA YA CHUNYA – TAARIFA YA KIFO.
MNAMO
TAREHE 16.12.2013 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
CHOKAA, KIJIJI CHA KIBAONI, KATA YA CHOKAA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA, EZEKIA D/O AZIGETI, MIAKA 10, MWANAFUNZI WA
DARASA LA PILI SHULE YA MSINGI CHOKAA, ALIKUFA MAJI WAKATI AKIOGELEA NA
WATOTO WENZAKE KWENYE MTO CHUNYA. CHANZO NI BAADA YA MAREHEMU KUZIDIWA
NA MAJI WAKATI AKIOGELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA
MAKINI NA WATOTO WAO HASA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA
KWA KUTOWARUHUSU KWENDA KUOGA KATIKA MITO/MABWAWA/MATIBWI YA MAJI. AIDHA
ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA/KUFUKIA NA KUZIBA MASHIMO NA VISIMA
VILIVYOWAZI ILI KUEPUKA MATUKIO YA WATOTO WADOGO KUFA MAJI.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE].
MNAMO
TAREHE 15.12.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
MANDA “B”, KIJIJI NA KATA YA GUA, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA CHUNYA, MKOA
WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA KWA USHIRIKIANO NA WAHIFADHI WA
HIFADHI YA NGWALA WALIMKAMATA OCTAVIAN S/O ISMAIL, MIAKA 38, MBUNGU
AKIWA NA SILAHA GOBOLE MOJA KINYUME NA SHERIA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI
HARAMU, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA
WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA KINYUME NA
SHERIA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment