Mechi
ya marudiano ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza fainali za
Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya
Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini (Batsesana) itachezwa Jumamosi,
Desemba 21 mwaka huu.
Mechi
hiyo itachezwa Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Johannesburg
kuanzia saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika Kusini. Tanzanite itaondoka
Jumatano, Desemba 18 mwaka huu saa 4 asubuhi kwa ndege ya Fastjet ikiwa
na msafara wa watu 29 wakiongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
TFF, Khalid Abdallah.
Kikosi hicho kitaagwa kesho (Desemba 17 mwaka huu) saa 6 katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Post a Comment