Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wa mikoa ya Simiyu, Mwanza na
Mara, Josephat Changwe, akimwongoza Waziri wa Maji , Profesa Jumanne
Maghembe (kulia) kuzindua moja ya visima 20 vya maji salama ya kunywa
vilivyokarabatiwa na kampuni hiyo kwa gharama ya sh.49.5 milioni,
wilayani Misungwi,Mwanza juzi.Anayepiga makofi (kushoto) ni Mbunge wa
jimbo la Misungwi, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira,
Charles Kitwanga.
Waziri
wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe (kulia), Naibu Waziri, Ofisi ya
Makamu wa Rais,Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Misungwi, Charles
Kitwanga (wa tatu kulia) na Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) wa mikoa ya Simiyu, Mwanza na Mara, Josephat Changwe wakisaidia
kumtwisha dumu la maji mmoja wa wanawake wa Kijiji cha Mapilinga, Wilaya
ya Misungwi, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa moja kati ya visima 20
vilivyokarabatiwa na TBL wilayani humo, kwa sh. mil 49.5.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa
Misungwi, Charles Kitwanga (kulia), akipampu maji huku Waziri wa Maji,
Profesa Jumanne Maghembe (pili kulia), na Mkurugenzi wa Sheria na
Uhusiano wa TBL, Steve Kilindo wakionja maji wakati wa hafla ya
kukabidhi visima vya maji 20 vilivyokarabatiwa na TBL wilayani Misungwi,
Mwanza, kwa sh. mil 49.5, juzi.
Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Bia (TBL),Stephen
Kilindo,wa kwanza kulia akitoa taarifa fupi ya ukaratabati wa visima 20
Wilayani Misungwi kwa Waziri wa Maji ,Profesa Jumanne Maghembe wa pili
kutoka kushoto.wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mariam Lugaila na
wa Kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mapilinga,Benard Busangu
juzi
Waziri
wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, akizungumza na mmoja wa wakazi wa
Kijiji cha Mapilinga Misungwi,baada ya kuzindua kisima cha maji kati ya
visima 20 vilivyoakaratbatiwa na Kampuni ya Bia (TBL) kwa sh.49.5
milioni.wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa TBL ,
Stephen Kilindo na Naibu Waziri Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais na
Mbunge wa Misungwi Charles Kitwanga.
Charles Kitwanga (kushoto) akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo muhimu.
Post a Comment