Kazi hiyo tuifanye sisi wenyewe. Jana
usiku sana nilimwona Rais wa Ghana John Dramani Mahama akihojiwa na CNN
kuhusiana na Mandela. Mara tatu Rais huyo wa Ghana aliutaja mchango wa
Tanzania katika ukombozi wa Afrika ikiwemo Afrika Kusini ya Nelson
Mandela.
-Hivi ni wangapi wanajua kuwa kiongozi
wa kwanza wa chama cha ukombozi katika nchi huru ya Kiafrika ambaye
Mandela alikutana nae anaitwa John Mwakangale. Huyu alikuwa kiongozi
katika TANU na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
-Hivi ni wangapi wanajua kuwa Mji wa
kwanza katika nchi huru ya Kiafrika ambayo Mandela alikanyaga ardhi yake
unaitwa Mbeya. Hivyo basi, Tanganyika ndio nchi huru ya kwanza ya
Kiafrika ambapo Mandela alikanyaga ardhi yake.(P.T)
- Hivi ni wangapi duniani wanajua,
kuwa Julius Nyerere ndiye Rais wa kwanza katika nchi huru ya Kiafrika
ambaye Mandela alikutana nae. Na ni Julius Nyerere baada ya kumkubali
Mandela, ndiye aliyemsaidia Mandela kwa kumtambulisha kwa Mfalme Haille
Selassie wa Ethiopia?
Haikuwa ajabu, kuwa baada ya kutoka gerezani, kwa Mandela Tanzania ikawa nchi ya kwanza kuitembelea.
Kumbukumbu hizi muhimu za kihistoria
na nyinginezo Watanzania hatupaswi kuisubiri CNN na vyombo vingine vya
habari vya kimagharibi viitangazie dunia.
Ni jukumu letu wenyewe.
Maggid Mjengwa.
Iringa.
Iringa.
Post a Comment