Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UZINDUZI RASMI WA MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2013 , KINGOLWIRA MOROGORO WAFANA

 

 Bwana Ali Masoud au Maarufu kwa Jina la’ Masoud Kipanya’ na ambaye Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus, akizungumza na wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2013 Kingolwira Morogoro , pia kumkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka kufanya uzinduzi huo.
 
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka, Akizungumza pamoja na wakazi wa eneo la Kingolwira pamoja na wageni mbalimbali waliotoka sehemu mbalimbali Tanzania na kutoa tamko rasmi la  kuzindua  shindano la Maisha Plus/ Mama shujaa wa chakula 2013
 
Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sister Matha Mwasu aliyeshika nafasi ya kwanza , Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2013, pia akieleza Jinsi alivyoweza kushinda na kupata mafanikio makubwa kutoka katika shindano la kizalendo la Maisha Plus.
 Mshindi wa Shindano la Maisha Plus Bernick Kimiro akizungumza na wageni wa alikwa pamoja na wenyeji wa eneo la Kingolwira Morogoro, kwa kuwasisitiza vijana wajitokeze kuchukua fomu za ushiriki katika shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2013 ambazo sasa zimesha anza kutolewa na kuwaeleza kuwa shindano hilo linatoa Fursa nyingi za kimaendeleo na kilimo kwa ujumla.
Mtaalam wa Mambo ya Mbogamboga na Mshauri katika maswala ya kilimo kutoka OXFAM Bwana Zephaniah akizungumzia kuhusiana na uzinduzi wa Maisha Plus/Mama shujaa wa Chakula 2013 , na kueleza faida za kilimo na kuwekeza kwa wakulima wodogo wadogo.
Dr. Emmanuel Tumusiime kutoka OXFAM akifanya uzinduzi rasmi wa Ripoti ya ‘Feed the Future Initiative in Tanzania’ ambapo katika ripoti hiyo kuna mambo ya msingi ya kulinda chakula kisije kikaja kuisha na Taifa likaja kukosa kabisa siku za mbeleni.
 
 Bwana Bonda ambaye ni mmoja wa wakurugenzi Maisha Plus
Kulia ni aliyekuwa Mshindi Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sr. Matha Mwasu akiwa na Mshindi wa Tatu Bi. Tatu
 
Kutoka Kulia ni Mshindi wa Pili wa wa Maisha Plus Venance Mushi akiwa na Mama shujaa wa chakula wa kwanza wa mwaka 2011 Bi. Ester Mtegule pamoja na Aliyekuwa mshiriki wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa chakula 2011 Bi. Dora Myinga
 
Mdau kutoka OXFAM Bill Marwa Akiwa anafuatilia kwa umakini uzinduzi wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2013
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Maisha Plus/ Mama shujaa wa Chakula 2013 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka  akifanya uzinduzi wa aina yake wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2012/13 kwa kufukua fomu ambazo zilikuwa zimefukiwa ikiwa ni kielelezo cha kilimo kwanza
  Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. AnthonyMtaka  akizionesha fomu hizo baada ya uzinduzi huo.
 
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka akimkabidhi Fomu ya kwanza ya ushiriki kwa Bi. Nuru Saidi Mbonga kutoka Dakawa ikiwa ni fomu ya Mama shujaa wa Chakula 2013
Mheshimiwa   Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka Akimkabidhi fomu ya Ushiriki wa Maisha plus kwa vijana Bi. Shamimu Ramadhani
 Mmoja ya Vijana wakiume nae akiwa anakabidhiwa fomu ya ushiriki na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka
Wakiwa wanasoma fomu na kujiandaa kuzijaza 
 
Waliovaa T-Shirt za Rangi nyeusi ni Wadau wa OXFAM
 
 Burudani za Ngoma zikiendelea
 Burudani za aina yake zikiendelea
 Wazee kutoka eneo la Kingolwira wakiwa wamekuja kushuhudia uzinduzi huo
 Wadau kutoka Sehemu mbalimbali wakiwa wamekuja shuhudia uzinduzi huo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus Ali Masoud ‘Kipanya’ akifunga sherehe fupi za uzinduzi wa Maisha Plus 2013
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top