Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Mstaafu Damian Libuva
(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano
wa NEC jijini Dares Salaam kuhusu tume hiyo iko huru. Kulia ni
Mkurugenzi wa NEC,Julias Malaba.picha na Magreth Kinabo – maelezo
……………………………………………………………………………………………………
Na Magreth Kinabo
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Mstaafu Damian Libuva
ametoa ufafanuzi kuwa tume hiyo iko huru na si kweli kwamba haiko
huru kama inavyonukuliwa katika baadhi ya taarifa na watu .
Kauli
hiyo imetolewa leo na Jaji Lubuva wakati alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC jijini Dares
Salaam, alisema tume hiyo iliundwa kwa mujibu wa sheria kupitia Iba
Jaji
Libuva alisema kwa muda mrefu katika chaguzi mbalimbali yamekuwepo
mlalamiko dhidi ya tume kuwa si huru na moja ya sababu zinazotolewa ni
kutokana na mfumo wa uteuzi wa makamishina wa tume kuchaguliwa na Rais,
ambaye ni kiongozi wa Chama tawala.
“
Hili linapigiwa kelele hasa na vyama vya siasa na wadau wengine wa
uchaguzi. Mara kadhaa katika mijadala limerudiwa rudiwa na hata baadhi
ya vyombo vya habari vimenukuliwa vikisema hata Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi amekiri kuwa tume siyo huru.
Tume
inafanya kazi zake za kusimamamia na kuongoza shughuli za uchaguzi kwa
uhuru ,na wazi bila kuingiliwa na chombo chochote iwe ni seriklai
au Chama chochote cha siasa,” alisema Jaji Lubuva.
Aliongeza kuwa tume hiyo haijawahi kuagizwa kuendesha uchaguzi kwa kupendelea chama au mgombea yeyote.
Aidha alisema katika mihadahra ambayo tume hiyo ilialikwa msimamo wa umekuwa ukitolewa ni Tume Huru.
“
Nimetoa mada katika vyuo vikuu Iringa na Dares Salaam ambapo uhuru wa
Tume umehojiwa katika mada hizo nimesisitiza juu ya suala hilo,”
alisisitiza .
Jaji
Lubuva alifafanua kuwa kwa vile mfumo uliopo wa tume hiyo ni wa
Kikatiba, kama wananchi na wadau kwa ujumla wanataka mfumo wa uteuzi wa
wajumbe wa tume ubadilike , basi wachukue fursa hiyo kutoa maoni yao kwa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Post a Comment