Mkuu
wa JWTZ msataafu Jenerali George Waitara (kulia) akimtunuku Mwenyekiti
wa TTB Balozi Charles Sanga cheti baada ya kushiriki kupanda mlima
Kilimanjarao katika kuadhimisha miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Anayeshuduia kushoto ni Mhifadhi Mkuu wa KINAPA Bwana Erastus Lufungulo
Jenerali
Waitara (kulia) akimtunuku cheti Meja Jenerali Christopher Gimongi
ambaye alikuwa kiongozi wa msafara wa wapanda mlima wa ‘Uhuru
Expedition’ mua mfupi baada ya wapanda mlima hao kukamilisha zoezi hilo
hapo jana.
Wapanda
mlima kutoka TTB, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakiwa
katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Jenerali mstaafu George Waitara
(mwenye jaketi jeupe), waongoza wapanda mlima, na Mkuu wa Hifadhi ya
KINAPA muda mfupi baada ya kukabidhiwa vyeti.
…………………………………………………………………………………………
Na Geofrey Tengeneza
Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la ulinzi
la Wananchi Tanzania-JWTZ Jenerali mstaafu George Waitara
ameihakikishia Bodi ya Utalii Tanzania –TTB kuwa Jeshi hilo litaendelea
kuunga juhudi za TTB katika kuvitangaza vivuto vya Utalii vya Tanzania
ukiwemo mlima Kilimanjaro kupitia msafara wa kupanda mlima Kilimanjaro
maarufu kwa jina la Uhuru Expedition unaofanywa na Jeshi la Wananchi kila mwaka katika kuadhimisha Uhuru wa Tanzania.
Jenerali Waitara ambaye ndiye Kiongozi na msimamizi mkuu wa Uhuru Expedtion
aliyasema hayo jana wakati akiwapokea wapanda mlima walioshiriki katika
msafara huo mwaka huu ulioratibiwa na kufadhiliwa na Bodi ya Utalii
Tanzania katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro –KINAPA Marangu
Moshi. “Tunaishukuru sana Bodi ya Utalii kwa kushirikiana nasi kwa mara
nyingine tene katika msafra huu, lakini pia nawashukuru sana KINAPA kwa
msaada wote waliotupa na niwahakikishie kuwa Jeshi litaendelea
kuutangaza utalii wetu wa Tanzania ukiwemo utalii wa kupanda mlima
Kilimnjaro” alisema Jenerali msataafu Waitara ambaye pia aliwakabidhi
vyeti wapanda mlima sita.
Mapema Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya TTB Balozi Charles Sanga ambaye pia alikuwa miongoni mwa
wapanda mlima alisema kuwa Bodi ya Utalii inafurahi kuona kuwa Uhuru Expedition
iliyoasisiwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania inaendelea kuimarika na
kutekeleza malengo ya kuanzishwa kwake na kwamba kwa kutambua mchango wa
Expedition hii ndiyo maana TTB imekuwa ikiiunga mkono. Amemsifia Jenerali Waitara kwa kuisimamia vema Expediton hii na kwa juhudi zake za kuhakikisha kila mwaka tukio la kupanda mlima la Uhuru Expedition linafanyika.
Naye Kiongozi wa Msafara uliopanda
mlima mwaka huu Meja Jenerali Christopher Gimongi amesema msafara huu
uliokuwa na wapanda mlima saba ulianza kupanda mlima tarehe 6/12/2013
kupitia njia ya Marangu na kwamba ni wapanda mlima watatu tu akiwemo
yeye walioweza kufika kileleni. Meja Jenerali Gimongi alisisitiza
umuhimu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kufadhili Uhuru Expedition kama alivyoahidi Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki wakati wa tukio kama hilo kama mwaka jana.
Tukio la kupanda mlima mwaka huu kupitia Uhuru Expedition
lilishirikisha wafanyakazi wawili wa TTB, Mwenyekiti wa TTB baolzi
Charles Sanga, Meja Jenerali Mstaafu Christopher Giomongi na wafanyakazi
watatu kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akiwemo
mwanamke mmoja.
Post a Comment