Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Shirika la Posta Tanzania lakusanya kiasi cha shilingi Bilioni 44.5 kufikia Mwaka 2012

 

Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta nchini Bw. Deus Mndeme akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mpango kabambe wa miaka 10 wa shirika hilo kupitia utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali pamoja na dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari bi. Zamaradi Kawawa.
 
Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara toka Shirika la Posta Bw. Fortunatus Kapinga akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya matumizi ya TEHAMA katika ofisi zake zipatazo 86 hapa nchini ili kutoa huduma kwa ufanisi.
 
Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa karibu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Deus Mndeme wakati akielezea mpango kabambe wa miaka 10 wa shirika hilo kupitia utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali pamoja na dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025.
 
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta nchini Bw. Deus Mndeme akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mpango kabambe wa miaka 10 wa shirika hilo kupitia utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali pamoja na dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025, Kushoto ni Meneja Mkazi Posta Zanzibar Bi. Mwanaisha Said.
(Picha na Eliphace Marwa)  
 
Na Frank Mvungi
 
Shirika la Posta Tanzania limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 44.5 kufikia mwaka 2012 ikiwa ni matokeo ya kuboreshwa kwa huduma zake hapa nchini.
 
Hayo yamesemwa na Posta Masta Mkuu Bw. Deos Mndeme wakati alizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mafaniko yaliyofikiwa na shirika hilo tangu kuanzishwa kwake.
 
Mndeme amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na huduma bora zenye hadhi ya kimataifa zinazotolewa na shirika hilo kwa wananchi hali itakayosaidia kuongeza mapato ya Serikali.
 
“Shirika limejipanga zaidi kutumia TEHAMA katika kuboresha huduma zake ikiwa ni moja ya mkakati utakaosaidia serikali kuongeza mapato na kufikia malengo ya muda mrefu yaliyowekwa na shirika pia tumejipanga kuendelea kuboresha huduma tunazozitoa ili kuendana na mahitaji ya wakati” alisema Mndeme.
 
Mndeme aliongeza kuwa kwa sasa shirika limeunganisha Ofisi 86 kwenye Wilaya na Miji kote nchini na mfumo wa mawasiliano ili kuongeza idadi ya wateja wanaohudumiwa,kuondoa ucheleweshaji na kuondoa  malalamiko ya wateja.
 
Katika kuhakikisha shirika linashiriki kikamilifu katika shughuli za kitaifa Mndeme alisema shirika litafanya uzinduzi wa toleo jipya la stempu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe hizo zitakazofanyika Disemba 28 mwaka huu.
  
Shirika la Posta ni mwanachama wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) ambalo Tanzania ilijiunga mwaka 1963 na kwa hivi sasa idadi ya nchi wanachama wa umoja huo ni 192 malengo ya Umoja huo ni pamoja na kuisimamia,utumiaji wa barua,Vipeto,Vifurushi katika nchi mbalimbali duniani,kutoa  ushauri,usuluhishi,kuunganisha ushirikiano baina ya nchi wanachama na kutoa misaada ya kiufundi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top