Wananchi
waliotaka kujichukulia sheria mikononi, nusura walichome moto gari la
wagonjwa lilitolewa msaada Kituo cha Afya Mtowisa wilayani Sumbawanga
mkoani Rukwa kutokana na madai ya kuchangia kifo cha mwalimu mmoja
aliyekosa msaada wa haraka wakati wa kujifungua.
Wananchi hao wanadaiwa kulishambulia gari hilo kwa mawe na kuvunja moja ya kioo.
Gari hilo
linadaiwa kuchelewa kuja kumchukua Mwalimu Leah Mgaya wa Shule ya
Msingi Mtowisa 'A', ambaye alifariki baada ya kutokwa na damu nyingi
wakati wa kujifungua.
Habari
kutoka sehemu ya tukio zilizothibitishwa na Ofisa Tarafa ya Mtowisa,
Peter Masindi zinaeleza kuwa, awali mwalimu huyo alipelekwa katika kituo
hicho cha afya juzi saa 3 asubuhi akiwa katika hali uchungu wa
kujifungua, lakini baadaye ilionekana anahitaji kupewa rufaa kwenda
Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa.
Masindi
alisema kutokana na hali hiyo ililazimu kupiga simu Ofisi ya Mganga Mkuu
wa Wilaya saa 6 mchana ili kuomba msaada wa gari, lakini gari hiyo
ilichelewa kufika kutokana na kudaiwa ilisafiri kwenda wilayani Nkasi,
na hata iliporejea jioni ilikwama njiani kutokana na hali ya mvua.
Mmoja ya
wananchi waliozungumza na gazeti hili, Mwaipungu alisema kifo cha
mwalimu huyo kiliwakera wananchi wa eneo hilo, ambapo walikusanyika
kwenye makundi na kuanza kujadiliana.
Wananchi hao walidai kuwa gari hilo la wagonjwa halina msaada kwani muda mwingi haliko kituoni hapo hivyo kutaka kulichoma moto.
Hasira za
wananchi hao zilionekana baada ya kufika kwa dereva wa gari hiyo
aliyefika, huku akiliza king'ora lakini alipokelewa kwa mabango, kabla
ya kumsimamishwa kumtaka kuwapa funguo za gari, jambo lililopingwa na
dereva. huyo huku wananchi hao wakilishambulia kwa mawe.
Post a Comment