Msanii
mahiri katika tasnia ya Filamu Bongo Hidaya Njaidi yupo katika wakati
mgumu kutokana na ajali aliyoipata kipindi cha nyuma ambayo imepelekea
mkono wake wa kushoto kuvunjika na kushindwa kupona ukiambatana na
maumivu makali.
“Kabla
hujafa hujaumbika mimi nilikuwa mtu wa kujituma katika shughuli zangu,
lakini tangu nipate ajali nimekuwa si uwezo huo, kwa sababu nashindwa
kufanya chochote yaani mkono wangu hauna nguvu ya kuinua hata kikombe
cha chai, imefika hatua hata nguo zangu za ndani nasaidiwa kufuliwa na
familia yangu, hata kuigiza naigiza nafasi chache ambazo ni za kawaida
maana sitakiwi kutumia nguvu , nimehangaika Hospitali kadha za hapa
Bongo lakini imeshindikana ushauri niliyopewa na Madaktari nikatibiwe
nje ya nchi,”alisema Hidaya.
Akizungumza na Maskani Bongo Msanii
huyo akiwa nyumbani kwake alisema kuwa ajali aliyoipata kipindi cha
nyuma imemrudisha sana nyuma katika kazi zake na kutafuta maendeleo
katika familia yake, ajali hiyo inamfanya ashindwe kuwa hata na furaha
kwenye jamii inayomzunguka.
Post a Comment