Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula akisoma hotuba ya ufunguzi
katika warsha ya kufunga mradi wa matumizi salama ya Bioteknolojia ya
kisasa katika Chuo ChaTaifa cha Utalii jijini Dar es Salaam
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (kushoto) akikabidhi kifaa
maalumu kwa Bw Haji Saleh, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kilimo – Zanzibar.
Kifaa hicho ni kwa ajili yakufanya tathmini na usimamizi angalifu wa bidhaa za mazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki.
Sehemu
ya Washiriki wa warsha ya matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa
wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mgeni rasmi (hayupo pichani).
Warsha hiyo ya kufunga mradi imefanyika leo katika Chuo cha Taifa cha
Utalii jijini Dares Salaam.
……………………………………………………………………………………..
EVELYN MKOKOI NA LULU MUSSAOFISI YA MAKAMU WA RAIS
DAR ES SALAAM
Bioteknojia
ya kisasa ni nyenzo mpya inayoweza kuboresha sekta mbali mbali za
kiuchumi zikiwemo sekta za kilimo, mifugo misitu, uzalishaji viwandani, na hifadhi ya mazingira.
Hayo
yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu
wa Rais Bw. Sazi Salula Katika ufunguzi wa Warsha ya kufunga mradi wa
matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa.
Bw.Salula
amesema kuwa, lengo kuu la teknnolojia hii ni kukidhi haja mbali mbali
za binadamu kama vile kuimarisha ubora wa mazao, kukidhi magonjwa,
kupata mbegu za mazao yanayohimili ukame na kukuza uzalishaji.
Aidha
aliongeza kuwa, pamoja na faida za bioteknolojia ya kisasa, bado kuna
wasiwasi kuhusu athari zinazoweza kutokea kutokana na bioteknolojia hii
ikiwa ni pamoja na uzio yaani allergy, kujitokeza kwa magugu sugu, saratani na usugu katika matibabu ya magonjwa.
Alisisitiza
kuwa, serikali imejiandaa kupunguza na kudhibiti athari hizi kutokana
na sababu kuwa Tanzania, haiwezi kukwepa athari zinazoweza kutokea
kutokana na muingiliano wa kimataifa hususan utandawazi
pamoja na mianya iliyopo katika mipaka na kuzingatia umuhimu wa matumizi
ya biteknolijia ya kisasa katika nchi yetu.
“si
kweli kwamba tanzania inakataa matumizi salama ya biteknojia ya kisasa
bali tunadhibiti ili kuepuka madhara yatokanayo na bioteknolojia ya
hiyo, Alisisitiza”
Bw.
Salula alianisha kuwa Tanzania kama nchi nyingine ni muhimu ikawa na
mfumo na vifaa vitakavyodhibiti bioteknolojia ya kisasa, ikiwa ni
wanachama wa mkataba wa Cartagena Tanzania inatakiwa kuweka taratibu
zitakazo hakikisha matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa.
Mradi
huu ulikuwa na lengo la kujenga uwezo kwa sekta na taasisi mbalimbali
zinazojihusisha na bioteknolojia ya kisasa ambapo maabara za taasisi
tano zilipatiwa vifaa vya kisasa vya kusaidia kutambua na kufanya
tathmini ya usimamizi angalifu wa bidhaa za mazao yaliyofanyiwa
mabadiliko ya kijenetiki.
Maabala
zilizonufaika na msaada huo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu
cha Kilimo cha Sokoine, Taasisi ya Utafiti na Kilimo – Zanzibar,
Taasisi ya Utafiti na Kilimo – Mikocheni na Mamlaka ya Chakula na Madawa
Tanzania.
Post a Comment