Katibu
Mtendaji toka Mradi wa Vitabu vya Watoto Bi. Pili Dumea akisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa
mzunguko wa sita tuzo kwa mashindano ya uandishi wa riwaya za kingereza,
kushoto ni Mratibu wa tuzo hizo Bw. Ramadhan Ali.
Katibu Mtendaji toka Mradi wa Vitabu vya Watoto Bi. Pili Dumea akionesha kitabu cha Run Free
cha mshindi wa kwanza wa tuzo za Burt katika mzunguko wa tano
kilichoandikwa na Richard Mabala, kushoto ni Mratibu wa tuzo hizo Bw.
Ramadhan Ali.
Katibu Mtendaji toka Mradi wa Vitabu vya Watoto Bi. Pili Dumea akionesha kitabu cha The Birthday Party cha
mshindi wa pili wa tuzo za Burt katika mzunguko wa tano kilichoandikwa
na Mukama Mwijarubi, kushoto ni Mratibu wa tuzo hizo Bw. Ramadhan Ali.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji toka
Mradi wa Vitabu vya Watoto Bi. Pili Dumea (hayupo pichani) wakati wa
uzinduzi wa mzunguko wa sita tuzo kwa mashindano ya uandishi wa riwaya
za kingereza.
Picha zote na Eliphace Marwa (MAELEZO)
……………………………………………………
Na Kiza Sungura-MAELEZO-Dar es salaam
Mradi
wa vitabu vya watoto Tanzania umezindua shindano la uandishi wa riwaya
za Kiingreza kwa ajili ya kuwajengea msingi wa kujifunza kwa urahisi
lugha hiyo vijana hapa nchini.
Shindano
hilo ni sehemu ya tuzo ya Burt ya fasihi ya kiafrika iliyoanza
kutekelezwa tangu mwaka 2008 na kwa mwaka huu ni mzunguko wa sita wa
mashindano ya uandishi wa riwaya za kiingereza kwa ajili ya vijana .
Akizindua
shindano hilo leo(jana) jijini Dar e salaam Katibu Mtendaji wa Mradi
huo Bibi Pilli Dumea amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuatambua
kazi nzuri zinazofanywa na waandishi wa fasihi barani Afrika na
kuwahamasisha waandishi wachanga waweze kushiriki katika ujenzi wa
fasihi .
“Lengo
la mashindano haya ni kutoa changamoto kwa waandishi na wasomaji wa
riwaya za kiingereza wa hapa nchini na Afrika kwa ujumla ili kuongeza
kasi ya usomaji na uandishi wa riwaya za kiingereza ili kuongeza uelewa
wa lugha hiyo”, alisema Bibi. Pilli.
Aidha
aliongeza kuwa mashindano haya yatakuwa na ushindani mkubwa kwani
yanashirikisha washiriki toka nchi nne ambazo ni wenyeji Tanzania,
Ethiopia, Ghana pamoja na Kenya.
“Mashindano
haya ya mzunguko wa sita yatakuwa na ushindani sana na zawadi ya
mzunguko huu ni dola za kimarekani elfu tisa kwa mshindi wa kwanza, dola
elfu saba kwa mshindi wa pili na dola elfu tano kwa mshindi wa tatu”,
aliongeza Bibi Pilli.
Alisema
kuwa mwisho wa kupeleka muswada wa riwaya itakuwa mwakani Mwezi Mei na
muswada huo unatakiwa uwe na maneno yasiyozidi elfu 20 na yasizidi elfu
40.
Muswada huo unatakiwa uwasilishwe kwa Mradi wa Vitabu vya Watoto Tanzania katika barua pepe yao ya childrensbook@gmail.com au nakala katika ofisi zao.
Post a Comment