Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WENGINE TENA WADAKWA NA MZIGO WA MIRUNGI WAKIISAFIRISHA

Jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi ndani ya viroba 30 yenye uzito wa kilo 30.
Mirungi hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutoka mjini Namanga kwenda wilayani Longido.
Akizungumzia jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni dereva wa gari hilo Zakayo Mwita mwenye umri wa miaka 26.
Aidha, alikuwa na mwenzake Juma Ramadhan mwenye umri wa miaka 24.
Kwa mujibu wa Sabas, watuhumiwa hao ni wakazi wa Namanga.
Sabas alisema watuhumiwa walikuwa wakitumia gari aina ya Noah.
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya raia wema kutoa taarifa kwenye kituo cha Polisi cha Ngaramtoni, ambapo askari waliokuwa doria waliweka mtego.
“Baada ya kupata taarifa, tuliweka doria na kufanikiwa kulikamata gari hilo na kukuta mirungi hiyo imefichwa sehemu mbalimbali ndani ya gari,” alisema Kamanda Sabas.

Sabas alisema wanaendelea kuwahoji watuhumiwa hao ili kubaini mtandao mzima wa wanaingiza dawa hizo kutoka nchi jirani.
“Kinachofanyika kwa sasa ni kuwahoji watuhumiwa ili kupata picha halisi ya mtandao mzima unaojihusisha na usafirishaji na uuzaji wa mirungi,” alisema Sabas.
 
MWANANCHI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top