MAREHEMU ZEINABU J KASENGA |
Rais
wa Serikali ya Wanafunzi CBE Dodoma Mhe, Remidius M. Emmanuel
alishiriki kwenye mazishi ya marehemu Zeinabu J. Kasenga katika makaburi
ya Wahanga (maili mbili) mnamo tarehe 24/12/2013.
Shekhe akimuombea Dua marehemu katika kaburi lake.
Baadhi
ya viongozi wa serikali ya wanafunzi (COBESO) walishiriki na wadau
mbalimbali wakiongozwa na Rais na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe, Dickson Msigwa (katikati) katika picha hii.
Watu walioshiriki kwenye mazishi
Mawaidha
ya kitolewa na shekhe (Hakuna anayejua siku wala saa kukutwa na umauti,
cha msingi ndugu zangu tujiandae, shukuru Mungu ukiona jua
linavyochomoza lakini inawezekana usione linavyo zama. Siku zote kifo
hakizoeleki) maneno ya Shekhe
Wadau
wakiwa na Rais wakizungumza jinsi msiba huu ulivyo wagusa, Mmoja wao
akisema chanzo cha kifo hicho ni maji, mnamo December 23 marehemu na
marafiki zake walienda kuogelea African Dream baada ya kuogelea ndio
akazama kama baada ya dakika mbili ndio kupata msaada wa kutolewa na
kupelekwa Hospital General, mnamo usiku wa kuamkia December 24 akapotea
maisha yake.
Post a Comment