Baadhi ya wananchi wakishuhudia ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 10:45 leo jioni katika eneo la Mlima Iwambi kuelekea Mbalizi |
Baadhi ya askari polisi wakilinda mali zilizokuwemo katika Lori, hata hivyo askari hao walilazimika kurusha risasi hewani kuwatawanya watu waliotaka kupora bidhaa hizo. |
Mmoja wa majeruhi wa ajali akiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya akisubiri kupatiwa matibabu. |
Wauguzi wa huduma ya haraka katika hospitali ya Rufaa Mbeya wakimpatia huduma mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo.(Picha kwa hisani ya Charles Abraham wa Malafyale Blog) |
WIMBI
la ajali katika miezi ya Disemba na Januari nchini limeendelea baada ya
ajali nyingine kutokea mkoani Mbeya leo jioni majira ya saa 10:45
katika mtelemko wa Mbalizi na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine 23.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ni kwamba magari mawili moja aina ya
Coaster na Lori la mizigo yalikuwa yakielekea njia ya Tunduma kutokea
Jijini Mbeya ambapo lori hilo linadaiwa kuharibika mfumo wa breki likiwa
mtelemkoni.
Lori
hilo la mizigo aina ya SCANIA lenye namba za usajili T 101 CRL na trela
lenye namba za usajili T 859 BZW ambalo lilibeba bidhaa mbalimbali za
madukani liliigonga Coaster yenye namba za usajili T 910 BFB na
kusababisha magari hayo kupinduka.
Post a Comment