Majeruhi wa ajali ya Bajaji Iringa
Karim Raphael (14) mkazi wa Mshindo ' A' katika Manispaa ya Iringa
akiwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Majeruhi wa ajali ya Bajaji Idd
Waziri Ng'eng'ena (17) mkazi wa kijiweni mjini Iringa akiwa na
majeraha usoni baada ya ajali hiyo mbaya ya Bajaji iliyosababisha
kifo cha dereva wa Bajaji hiyo
Muuguzi katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa akimpatia matibabu majeruhi Karim
Idd na Karim wakisubiri kupelekwa wodini baada ya kupatiwa matibabu ya awali OPD |
AJALI mbaya ya Bajaji
yasababisha kifo cha dereva wake ambae ni mfanyakazi wa maduka ya
Mzalendo mjini Iringa Bw Sudi Hashimu (22) mkazi wa Mtwivila huku wengine wawili wakijeruhiwa
vibaya.
Ajali hiyo mbaya imetokea majira ya saa 2 usiku wa
kuamkia leo katika
eneo la Mshindo mjini Iringa
wakati dereva huyo wa Bajaji
akijaribu kukimbia baada ya kudaiwa
kusababisha ajali katika eneo la
Miyomboni mjini Iringa.
Wakizungumza na mtandao wa www.matukiodaima.com majeruhi wa
ajali hiyo Karim Raphael na Idd Waziri
Ng’eng’ena walisema kuwa kabla ya ajali hiyo
dereva huyo alikuwa amesababisha
ajali kwa kumgonga mwendesha Bajaji
mwenzake na baada ya tukio hilo aliamua
kutimua mbio kwa kutumia usafiri wake wa Bajaji.
Kwani walisema
kufuatia ajali hiyo eneo la Miyomboni
ulizuka ugomvi kiasi cha aliyegongwa kupokonya
kofia (Helmenti) ya Bajaji ya
Sudi kabla ya marehemu huyo kufanikiwa kupokonya na kukimbia .
“Katika Bajaji
marehemu alikuwa ametupakia abiria
watatu ambapo mmoja aliruka kabla ya
Bajaji hiyo kuchanganya zaidi
hivyo tukabaki abiri
wawili na dereva mwenyewe …hata hivyo alionekana kuendesha
Bajaji hiyo kwa sifa zaidi na kuonyesha kuwa
yeye ni bingwa wa kukimbiza
Bajaji hiyo” alisema majeruhi Karimu
Hata
hivyo alisema
baada ya kufika eneo la Mshindo Kanisani katika tuta
kubwa dereva huyo alishindwa kupunguza mwendo na hivyo kulivaa tuta
hilo wakati akitaka kukata kona na Bajaji hiyo kuacha njia na kugonga
ukuta wa uzio wa
Kanisa la RC mshindo na dereva huyo
kutanguliza kichwa katika ukuta huo
huku wao
wakifunikwa na Bajaji hiyo.
Walisema kuwa
dereva huyo alikufa papo hapo huku wao wakishuhudia
kifo chake kabla ya wasamaria
wema kufika na kuwaokoa.
Kwa upande wake
mmoja kati ya shuhuda wa
tukio hilo Mood Mambo alisema
kuwa alifika eneo hilo na kukuta wananchi
wakiendelea kutoa msaada kwa watoto hao ambao walikuwa wamejeruhiwa
vibaya na mwili wa marehemu ukiwa
umepasuka kichwa .
Majeruhi hao
walikimbizwa katika Hospital ya
rufaa ya mkoa wa Iringa huku mwili wa marehemu huyu ukihifadhiwa katika chumba cha maiti
katika Hospital hiyo.
Ajali hiyo ni ya pili
kusababisha kifo kwa mkoa wa Iringa na ajali ya tatu mbaya
kutokea katika mkoa wa Iringa toka mwaka 2014 ulipoanza ambapo ajali ya
kwanza kusababisha kifo ilitokea wilaya ya Mufindi nay a pili
kujeruhi ilitokea eneo la Ilala wakati wa mkesha wa Mwaka mpya ikiwa ni dakika
20 kuukaribisha mwaka mpya na kupelekea dereva wa boda boda kukatwa mguu wake nah ii ni ya tatu .
Hata hivyo ajali hizo
zimeendelea kutokea mbali ya kuwepo jitihada
kubwa zinazoendelea kufanywa na
kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa chini ya mwenyekiti wake Salim Asas katika kutoa
elimu ya usalama barabarani kwa madereva
boda boda mkoa wa Iringa ila bado ajali za boda boda zaendelea kutoa roho za
vijana wanaofanya kazi hiyo
Sikiliza Video hii chini Shuhuda Karim anavyoshuhudia ajali hiyo na jinsi walivyopona kifo
Sikiliza Video hii chini Shuhuda Karim anavyoshuhudia ajali hiyo na jinsi walivyopona kifo
Post a Comment