Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu leo amekabidhi tiketi na hati nyingine
muhimu kwa vijana wanne wa Tanzania kwa ajili kuondoka leo kwenda Dubai,
kufanya kazi za ajira kupitia Kampuni ya Bravo Job Centre Agency Ltd.
Pichani Mtemvu akimkabidhi hati, mmoja wa vijana hao, Zainab Suleiman
mkazi wa Buza Dar es Salaam, katika hafla iliyofanyika, jijini Dar es
Salaam. Wengine wanaosubiri kupata hati hizo ni Zuhura Ismail mkazi wa
Keko, Maimuna Ibrahim na Aziza Seleman wote wakazi wa Yombo.
Wanaoshuhudia ni Maofisa kutoka Kampuni ya Bravo, Mohamed Said na
Khalifa Mayamba. Akizungumzia hatua hiyo ya kuwapeleka Vijana wa
Kitanzania kwenda kufanya kazi Dubai, Mtemvu amesema, Wale wote
waliokwishapelekwa huko kupitia Kampuni ya Bravo, hakuna aliyepatwa na
matatizo kidiplomasia au kudhalilishwa kama ambavyo baadhi ya vyombo vya
habari vimeanza kuripoti.
Mbunge huyo amesema, kutokana na Bravo kuhakikisha taratibu zote zinakuwa sahihi, wale wote waliokwishapelekwa huko wanaendelea vizuri.
Amesema, kama wapo wanaopatwa na matatizo ya kidiplomasia au kunyanyaswa ni Vijana wanaopelekwa au kwenda huko kwa njia za panya.
"Sisi tumekuwa tukizingatia taratibu zote, kwa hiyo si rahisi mtu tuliyempeleka huko akapata matatizo, yaliyo nje ya taratibu za ajira yake. Na hao wanaoandika kwamba waliopelekwa huko wanadhalilishwa basi hao hawatuhusu sisi, siyo waliopitia mikononi mwetu", alisema Mtemvu.

Post a Comment