Habari zisizo njema kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano ni kwamba mbunge wa Chalinze Mh. Said Bwanamdogo anaumwa hoi mahututi akiwa amelazwa katika chumba maalumu kwa wagonjwa wanaopewa uangalizi maalum (ICU) MOI.
Chanzo cha habari hizi kiliwashuhudia baadhi ya wabunge wa mkoa wa pwani wakiwa pale MOI kumjulia hali mwenzao. Wabunge walioonekana maeneo hayo ni pamoja na Dr Seif Rashid Rufiji na naibu waziri wa afya pamoja na Mh Koka mbunge wa Kibaha mjini.
Duru za uhakika zinaeleza kuwa Mh Bwanamdogo amekuwa mgonjwa kwa kipindi kirefu na juhudi za kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu bado hazikuzaa matunda mpaka kufikia uamuzi wa kumrudisha nchini.
Tumwombee mbunge wetu apate nafuu. Amen.
Post a Comment