Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CCM NA CHADEMA WAZINDUA KAMPENI YA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KIBORILONI KWA KISHINDO

 


SAM_0309
Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Michael Mwita (Kushoto)
akiteta jambo na Mgombea wa kiti cha Udiwani kata ya Kibor0loni kwa
tiketi ya chama cha Mapinduzi, Willy Adriano, wakati wa Uzinduzi wa
Kampeni kuelekea uchaguzi mdogo kuziba pengo lililoachwa wazi na
aliyekuwa Naibu Meya na Diwani wa Kata hiyo,, Marehemu Vincent Rimoy
aliyefariki dunia Novemba 6, mwaka jana.
SAM_0314Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanajro, Iddi Juma,
(aliyeshika kipaza sauti), akimnadi mgombea wa CCm katika Uchaguzi
mdogo wa Udiwani, Wlly Adriano katika uchaguzi uzinduzi wa kampeni za
uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Februari 9 mwaka huu kuziba pengo
lililoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwanbi wa Kata ya
Kiborloni, Vincent Rimoy, alyefariki dunia ghafla Novemba 6 mwaka
jana.
 SAM_0318
Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi (kushoto), akiwa
akimtambulisha Mgombea wa Udiwani katika kata ya Kiboriloni, Willy
Adriano aliyesimama katikati, kulia kwake ni Mke wake.(Picha zote na
Taifa Letu.com Blog)

…………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Moshi
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), mwishoni mwa wiki walifanya uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi
 mdogo wa udiwani katika kata ya Kiboriloni liliachwa wazi kufuatia
kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Vincent Rimoy (CHADEMA),
aliyefariki ghafla Novemba 6 mwaka jana.
Wa kwanza kufanya uzinduzi ni Chadema, waliozindua kampeni yao kwa
mbwembwe wakimtambulisha mgombea wao, Frank Kagoma ambaye ni
mwenyekiti wa mtaa wa Mnazi, uzinduzi ulioongozwa na viongozi
mbalimbali wa ngazi za juu wa chama hicho mkoani hapa akiwemo
mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge wa Jimbo la Moshi
mjini, Filemon Ndesamburo.
Wakizungumza katika Nyakati tofauti katika uzinduzi huo uliofanyika,
Jumamosi ya Januari 18, mwaka huu, katika stendi ya kidia, viongozi wa
Chadema walianza kumnadi mgombea wao ambap[o walimtaja kama mtu sahihi
ambaye anaweza kuendeleza mapambano ya chama hicho ndani ya baraza la
madiwani kupinga ufisadi na uonevu katika manispaa ya Moshi.
Meya wa Manispaa ya Moshi, Jafari Michael, aliwataka wananchi wa kata
hiyo kumchagua mgombea wa Chadema kwani ndiye mwenye uwezo wa
kutekeleza yale yote aliyoyaanzisha Marehemu Rimoy ndani ya kata hiyo
na baraza la madiwani.
“Wananchi wa kiboriloni msidanganyike, chaguo la kweli katika
maendeleo ya kata hii ni Kagoma, katika kipindi chake kama mwenyekiti
Kagoma alifanikiwa kuvunja magenge yote ya ujambazi na sasa mnatembea
vifua mbele bia wasiwasi, tupeni kagoma tuendeleze moto wa Chadema
ndani ya Baraza la Madiwani, tupeni kagoma tukamalizie kazi
aliyoianzisha Rimoy,” alisema Rimoy.
Naye Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Filemona Ndesamburo alisema kazi
ya kuleta maendeleo katika kata hiyo na mkoa kwa ujumla  unaweza
kufanywa na watu makini wenye uthubutu kama alivyo na uthubutu Mgombe
wa kiti hicho, Frank Kagoma.
Kwa upande wao, Chama cha Mapinduzi CCM, waliofanya uzinduzi wao juzi,
kwa kumtambulisha mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya CCM, Wlly
Adriano walisema Maendeleo ya kata ya Kiborloni ni zaidi ya itikadi za
siasa na kuwataka wananchi wa kata hiyo kufanya uamuzi sahihi.
Akizungumza na maelefu ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya
stendi ya Kidia, Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi
alisema wapo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitafuta madaraka
kwa njia mbalimbali, ikiwemo  kufanya vurugu na maandamano.
 “Unajua ukisikia nchi fulani ina maendeleo kiuchumi, kisiasa na mambo
mengine ni kwa sababu kuna amani, kwa hiyo hili jambo ndugu zangu ni
muhimu sana kulizingatia ili kutuwezesha kuendelea na kazi zetu za
kijamii vizuri” alisema Kazidi.
Kwa upande wake Mchumi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Paul Matemu,
aliwataka  vijana kutokuuza shada zao za kupigia kura kwani kufanya
hivyo ni kuuuza maendeleo yake.
Aidha Matemu aliongeza kwa kusema  kuwa siasa bila maendeleo hakuna
kujenga msingi wa kuleta maendeleo, na kuwataka wananchi wa kata ya
kiboriloni kuchagua Willy Adriano ili aweze kuwawakilisha katika
baraza la madiwa la Manispaa ya Moshi.
Naye Mgombea udiwani kwa tiketi ya chama hicho, Willy Adriano, alisema
Siasa za Tanzania haziwezi kupiga hatua endapo wananchi hawatabadilika
na kuacha tabia ya kuchaguana kwa kuangalia kigezo cha itikadi za
kisiasa.
Uchaguzi mdogo wa udiiwani  katika kata ya Kiboriloni uunarajiwa
kufanyika Februari 9 mwaka huu kuziba pengo lililoachwa wazi kufuatia
kifocha aliyekuwa diwani wa kata hiyo kwa tikiketi ya chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Vincent Rimoy.
Rimoy ambaye alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi, alifariki dunia
ghafla, Novemba 6 mwaka jana, baada ya kudondoka akiwa shambani kwake
eneo la mandaka wilaya ya Moshi
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top