Pikipiki ikiwa chini ya uvungu wa gari baada ya kuburuzwa
Dereva wa pikipiki hiyo Bw Ndiba akihojiwa
Polisi wakiwasili eneo la tukio.
Na Dustan shekidele,morogoro
DEREVA wa
boda boda Anthony Kalikana'Ndiba' juzi kati amenusurika kifo baada ya
pikipiki aliokuwa akiendesha kugongwa kwa nyuma na kubuluzwa umbali wa
mita 200 na daladala eneo la Sido barabara kuu ya Msamvu mjini.
Akisimulia
tukio hilo Ndiba alisema" bahati siku na abiri kama ningekuwa na abiria
angekufa papo hapo kwani jamaa alikuja kwa kasi nyuma yangu na kwamba
tulipofika hapa Sido jirani na kanisa la KKKT Mji Mpya amenigonga kwa
nyumba na kunirusha bahati mbele kulikuna na gari nikaluka na kuidandia
gari ile na kunusulika bila hivyo jamaa angenitoa roho"amesema kwa
uchungu boda boda huyo na kuongeza
''Baada
ya tukio hilo dereva wa hii daladala alikimbia na mimi kwa hasira
nimechukua funguo na kwamba gari haitoki mpaka nilipwe,kifupi mimi ni
komandoo sijaumia popote lakini chombo changu kama unavyokiona kipo
chini ya uvungu gari kimeburuzwa toka pale kanisani mpaka hapa ofisi za
Hood"alisema Ndiba
.
Baada ya
muda polisi walifika eneo la tukio na kuchukua pikipiki hiyo pamoja na
daladala hiyo ambayo iliendeshwa na dereva mwingine kueleka kituo cha
polisi.
Post a Comment