Jeshi
la Polisi Zanzibar linamshikilia Askari mmoja wa Chuo cha Mafunzo sawa
na Magereza kwa Tanzania Bara kwa tuhuma za wizi wa shilingi 1,635,000
alizoziiba kutaka katika duka moja lililopo eneo la Makadara mjini
Zanzibar.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Mkadam Khamis Mkadam, amemtaja Askari huyo kuwa ni Sajin Meja (S/Sgt) Hassan Iddi Hassan (45), wa Chuo cha Mafunzo Makao Makuu.
Kamanda
Mkadam amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.00 jioni
ambapo Askari huyo akiwa amevaa kiraia, alifika dukani hapo kama mteja
wa kawaida na wakati muuzaji wa duka hilo akimhudumia mteja mwingine
upande wa pili, aliingia ndani na kukimbilia kwenye droo ya pesa na
kuzichukua fedha hizo na kuondoka.
Amesema
wakati akichukua fedha hizo, Askari huyo alionwa na baadhi ya wateja na
hivyo kumshitua muuzaji huyo na kuanza kupiga kelele za mwizi na ndipo
alipofukuzwa na wananchi na kwa vile eneo hilo lilikuwa karibu na Kituo
cha Polisi askari waliwahi haraka na kumkamatwa kabla ya kupata kipigo
kikali kutoka kwa wananchi.
Kamanda
Mkadam, amesema fedha zote alizokua ameziiba mtuhumiwa huyo zimeokolewa
na Polisi na zimehifadhiwa kama kielelezo mahakamani.
Hilo
ni tukio la tatu kutokea mjini Zanzibar katika kipindi cha mwaka huu
ambapo tukio la kwanza ni lile la jaribio la wizi katika maghala ya
Bakheresa eneo la Fuoni nje kigodo ya mji wa Zanzibar ambapo watuhumiwa
watatu walikamatwa wakiwa na silaha aina ya gobore linalotumia risasi za
short gun.
Na
tukio linguine ni la kukamtwa kwa majambazi wanne akiwemo Afisa wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini wakiwa na silaha tatu
zikiwemo bastola mbili na SMG moja baada ya kumvamia mfanyabiashara
mmoja na kumpora milioni 11.5 eneo la Rahaleo mjini Zanzibar.
Matukio
hayo yote yakiwa na jumla ya watuhumiwa wanane na silaha nne yaliweza
kukabiliwa kwa haraka na Polisi kufuatia msaada wa wananchi wa kutoa
taarifa za haraka polisi na wenyewe kujitolea kusaidiana na Polisi
kuwakabili watuhumiwa na kufanikisha ukamataji salama.
Post a Comment