Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua kazi ya uwekaji viti vipya katika
ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Januari 18,2014 ikiwa ni maandalizi ya
Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao. (Picha na Ofisi
yaWaziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua marekebisho yanayofanyika katika ukumbi wa
Bunge mjini Dodoma Januari 18, 2013 ikiwa ni maandalizi ya Bunge la
Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua marekebisho yanayofanyika katika ukumbi wa
Bunge mjini Dodoma Januari 18, 2013 ikiwa ni maandalizi ya Bunge la
Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
……………………………………………………………………….
*Ni maandalizi ya Bunge la Katiba
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema ameridhishwa na kazi ya ukarabati
inayoendelea kwenye maeneo mbalimbali ya jengo la Bunge ikiwa ni
maandalizi kwa ajili ya Bunge la Katiba.
“Maendeleo
ni mazuri na kazi inayofanywa ni nzuri, kikubwa ni kuhakikisha
mnaikamilisha hii kazi katika muda uliopangwa,” alisisitiza.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumamosi, Januari 18, 2014), wakati
akipokea maelezo ya ukarabati kutoka kwa Mhandisi Mkuu wa Ofisi Bunge,
Eng. Dk. Philemon Mzee ambaye alikuwa akimtembeza kwenye maeneo
mbalimbali yanayofanyiwa ukarabati. Kwa mujibu wa Dk. Mzee, kazi hiyo
inatarajiwa kukamilika Januari 30, mwaka huu.
Ndani
ya ukumbi wa Bunge, Waziri Mkuu alikuta viti vyote vya zamani
vimekwishaondolewa na akaonyeshwa sehemu moja ya mfano iliyopangwa viti
vinane kuashiria muonekano utakavyokuwa mara baada ya kazi hiyo
kukamilika.
Dk.
Mzee alimweleza Waziri Mkuu kwamba wanatarajia kuweka viti 670 vya
wajumbe wa kawaida pamoja na viti 24 kwa ajili ya wajumbe wenye mahitaji
maalum. “Kule nyuma tutaweka viti vya kuzunguka ili hata kama mjumbe
mmoja ana ulemavu wa miguu na amekuja na baiskeli yake aweze kutoka na
kukaa kwenye kiti chake kwa urahisi,” alisema.
Alimweleza
Waziri Mkuu kwamba viti vya Spika na Makatibu wa Bunge vipo tayari,
mfumo wa vipaza sauti uko sawa na kwamba kila kipaza sauti kimoja
kitakuwa kinatumiwa na watu wawili kulingana na mpangilio wa ukaaji
ulivyo.
Alipoulizwa
na Waziri Mkuu kuhusu sehemu ya kukaa waandishi wa habari, Eng. Mzee
alisema sehemu zao zitaendelea kubaki zilivyo. Alipohoji endapo kutakuwa
na kazi za Kamati, zitafanyikia wapi, Waziri Mkuu alijibiwa kwamba kuna
kumbi tisa za kutosha watu 25-30 zinaandaliwa katika jengo la utawala
Annex.
Waziri Mkuu pia alikagua sehemu ya mgawaha kwa ajili ya wajumbe wa bunge hilo na kuonyeshwa sehemu ya basement
ambayo alikuta inafanyiwa matengenezo ili iweze kuchukua watu 500 kwa
wakati mmoja. Pia alikagua mgahawa wa zamani wa bungeni na kuelezwa
kwamba utatumiwa na watumishi tu na hivi sasa unafanyiwa ukarabati ili
uweze kutosha watu 120 kwa wakati mmoja.
Waziri Mkuu alikagua pia chumba cha Hansard
ambako alielezwa kuwa kimeongezwa ili kiweze kutosha watumishi 80
ikilinganishwa na watumishi 25 waliokuwepo zamani. Pia alikagua server room ambayo imehamishiwa eneo yalipokuwa matawi ya benki na zahanati.
Alipouliza
kuhusu eneo la kuegeshea magari, Waziri Mkuu alielezwa kwamba
limetengwa eneo la kutosha magari 400 ambalo hivi sasa linafanyiwa
maandalizi.
Katika
jengo la Utawala Annex, Waziri Mkuu alielezwa jengo hilo litakuwa na
ofisi, vyumba vya mazoezi (gym), zahanati na ofisi za kutolea huduma za
kibenki.
Akitoa
maelezo kuhusu kazi ya ukarabati inayoendelea, Kamishna Msaidizi wa
Magereza ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa jengo la Utawala Annex, Eng.
Salum Omari alisema walianza kazi hiyo Januari 2, mwaka huu na
wanatarajia kuikamilisha ifikapo Februari 2, mwaka huu.
Alipoulizwa
kama watamudu kuikamilisha kazi hiyo katika tarehe iliyopangwa, Eng.
Omari alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba wataikamilisha katika muda huo.
Waziri Mkuu amerejea jijini Dar es Salaam mchana huu.
Post a Comment