Rais
Mstaafu wa Tanzania Mzee Mwinyi akimkabidhi Zawadi za Juzuu, Mashafu ,
vyeti pamoja na tuzo Maalum Mgeni Rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye hafla ya kuzaliwa Mtume Muhammad
(SAW) yaliyofanyika Mtaa wa Msimazi Kariakoo Jijini Dar es salaam.
Wanamadrasat
Nurul Huda wa Tandika Jijini Dar es salaam wakifanya vitu vyao wakati
wa hafla ya kisomo cha mazazi ya Mtume Muhammad (SAW) kilichofanyika
katika ukumbi wa wapenzi wa Mtume Muhammad (SAW) wa Chaurembo wa Mtaa wa
Msimbazi Kariakoo Jijini Dar es salaam.
Mwana
Umoja wa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } wa Chaurembo wa Mtaa wa
Msimbazi Rais Mstaafu wa Tanzania Al- Hajj Mzee Ali Hassan Mwinyi akitoa
salamu zake wakati wa kisomo cha mazazi ya Mtume Muhammad (SAW) hapo
Mtaa wa Msimbazi Mjini Dar es salaam. Kulia
ya Mzee Mwinyi ni Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kushoto ya Mzee Mwinyi ni Mkurugenzi
wa Kituo cha Kiislamu Tandika Dar ves salaam Sheikh Usama Ismail.
***********************
Waumini wa Dini ya Kiislamu popote walipo katika kipindi hichi cha kusherehekea uzawa wa Kiongozi wa
Dini hiyo Ulimwenguni Mtume Muhammad { SAW } wana wajibu wa kupitisha
maazimio ndani ya nafsi zao ya kuachana na maovu na kukumbatia mema yote
kama alivyokuwa akiyahubiri Kiongozi huyo wakati wa uhalifa wake.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo katika
kisomo cha mazazi ya Mtume Muhammad { SAW } kilichofanyika katika ukumbi
wa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } wa Chaurembo waliopo katika Mtaa
wa Msimbazi Kariakoo Mjini Dar es salaam.
Balozi
Seif alisema mkusanyiko wa waumini wa Kiislamu katika kutukuza uzawa wa
Kiongozi wao utakuwa na manufaa makubwa endapo kila muumini atadhamiria
kusoma kwa kina maisha ya kiongozi huyo kwa lengo la kufuata mwenendo
wake.
Alitoa
wito kwa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } kufanya utafiti mbali mbali
zitakazotoa fursa kwa waumini wa dini ya Kiislamu popote pale kusoma na
hatimae kuelewa vyema maisha na mfumo aliokuja nao Kiongozi huyo wa
umma wa Kiislamu.
“
Ikiwezekana tafiti hizo ni vyema zikaandikwa kwa lugha ya Kiswahili ili
watu wengi zaidi wapate kuzisoma. Kuelewa maisha ya Mtume Muhammad {
SAW } ni hatua muhimu kwa muumini wa Kiislamu kuielewa Dini yake “.
Alisisitiza Balozi Seif.
“ Akinukuu
baadhi ya maandiko yaliyotolewa na wanafalsafa wa Dini ya Kiislamu
Balozi Seif alisema kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad { SAW } ni
sawa na kusherehekea kuzaliwa kwa Uislamu “.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwasisitiza waumini wa Dini ya Kiislamu
kuendelea kuwa na utiifu, subra wakati wa matatizo sambamba na
kujijengea maisha bora ya milele ambayo kila muumini anayaelewa.
Balozi
Seif alielezea faraja yake kutokana na uwepo wa Umoja wa wapenzi wa
Mtume Muhammad { SAW } hapa Tanzania ambao unastahiki kupongezwa pamoja
na kuungwa mkono .
Alisema
jamii katika kipindi kirefu ilikuwa ikishuhudia kuwepo kwa umoja wa
wapenzi wa vilabu vya mchezo wa mpira wa miguu au wanamuziki badala ya
kuwa na umoja kama huo unaoleta faida pande zote mbili Duniani na Makazi
ya milele.
“
Maandalizi ya sherehe hiziyameonyesha wazi kwamba nyinyi kweli ni
wapenzi wa Mtume Muihammad { SAW }. Tunamuomba Mwenyezi Mungu
atuzidishie mapenzi yetu kwa kiongozi wetu huyo “. Alifafanua Balozi
Seif.
Akitoa
salamu kwenye hafla hiyo ya kisomo cha mazazi ya Mtume Muhammad {
SAW } Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi alisema waumini wa Dini ya Kiislamu
wana wajibu wa Kumshukuru Mola kwa kuupatia umma huu wa mwisho Kiongozi
aliyekamilika kwa tabia, nasabu pamoja na Umbo.
Mzee
Mwinyi aliwataka waislamu hao kuendelea kuheshimu nema walizopewa na
Mwenyezi Mungu za kupatia Kitabu kitukufu na bora chenye mfumo kamili wa
kufuatwa na wanaadamu katika maisha yao ya kila siku.
Mapema
Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislamu kilichopo Tandika Mjini Dar es salaam
akiwa miongoni mwa matunda ya chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha
Al – Akhzal nchini Misri Sheikh Usama Ismail alisema dalili za utukufu
wa Mtume Muhammad { SAW } zilianza kujichomoza tokea zama za Mitume
waliomtangulia.
Sheikh
Usama alifahamisha kwamba Kiongozi huyo wa Umma wa Kiislamu
alibashiriwa utukufu wa kuja kwake duniani ambao baadhi ya maulamaa wa
enzi zilizopita waliushuhudia ndani ya vitabu vitukufu.
Katika
hafla hiyo ya kisomo cha mazazi ya Mtume Muhammad { SAW } Muasisi wa
Umoja wa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } wa Chaurembo waliopo katika
Mtaa wa Msimbazi Kariakoo Sheikh Majid aliwapongeza Viongozi hao kwa
ukaribu wao na waumini pamoja na wananchi kwenye masuala mbali mbali ya
kijamii.
Katika
kuunga mkono harakati za kijamii zinazofanywa na viongozi hao Sheikh
Majid kwa niaba ya Umoja huo alikabidhi zawadi za Juzuu, Mashafu pamoja
na hati maalum kama ukumbusho kwa wageni hao waalikwa akiwemo pia Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al Hajj Daktari Ali
Mohamed Shein.
Post a Comment