Habari mbaya leo kwenye michezo ni
kuhusu majeraha ya mshambuliaji Radamel
Falcao aliyoyapata jana usiku kwenye mchezo kati ya timu yake ya Monaco dhidi
ya timu ya ligi daraja la nne ya Chasselay kwenye kombe la Ufaransa.
Kwenye mchezo huo Falcao alifungia bao
la kuongoza wakati timu yake ya Monaco ilipopata ushindi wa mabao 3-0
kabla ya kuumia, taarifa zilizotoka leo baada ya vipimo zinasema jeraha
hilo litamuweka nje kwa
kipindi cha miezi sita na kupelekea kuzikosa fainali za kombe la dunia baadae mwezi wa sita
nchini Brazil.
Kukosekana kwa Falcao kwenye mashindano
hayo sit u pigo kwa nchi yake ya Colomboa bali litakuwa pigo kwa mashindano
hayo kumkosa mshambuliaji huyo.
Post a Comment